Tuesday, January 29, 2013

MFUMO WA DIGITAL UMENIVUNJA NGUVU NA KUNIPUNGUZA SPEED

Licha ya kufanya karakati za kutengeneza video mpya ya wimbo wake "yatakwisha" aliyofanya na lina, ambayo mpaka hivi sasa ipo katika hatua za mwisho, Ben pol amesema mfumo wa digital umemvunja nguvu na kumpunguzia kasi, kwasababu kumekuwa na mvurugano kwenye televisheni zetu na hivyo kuwa sio kipindi kizuri cha kufanya biashara, maana watu wengi kama asilimia 85 hawana access ya kuona video kwa ufasaha, kwahiyo anaweza akaipoteza tu video hiyo.
 
"nafikiri kuanzia march au april ndio nitatoa maana naamini vitu vitakua vimenyooka, kiujumla nimepanga nitoe video mbili kwa mwaka huu, moja nitoe mwanzoni na nyingine iwe juu ya mwezi wa sita, either wa nane au wa tisa." amesema Ben Pol.

No comments:

Post a Comment