Sunday, March 31, 2013

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi:' Watu waliyoko karibu na jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi wa kwanza aliyejenga jengo la ghorofa 16 na Kuporomoka Nakusababisha vifo vya Watu 22 ,kuhama mara moja na ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara.'

Picha Juu ni jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi aliyesababisha jengo la ghorofa 16 kuanguka na kusababisha vifo vya watu 22 hadi sasa ambalo waziri lukuvi ametoa maelekezo kubomolewa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
---
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
 
Habari zilizopatikana kutoka eneo la uokoaji na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova zinaeleza kuwa miili iliyopatikana imepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya Lucky Construction Limited liliporomoka saa 2.30 asubuhi wakati mafundi na vibarua wakiendelea na ujenzi huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao kama kawaida.

No comments:

Post a Comment