TAARIFA:::IDADI YA WATU WALIOKUFA MPAKA SASA NI 18 KWENYE JENGO LILILODONDOKA JANA.
Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka jana asubuhi katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam. |
Watu wa Msalaba Mwekundi wakibeba moja ya majeruhi wa tukio hilo |
WAKATI zoezi la
uokozi kwenye tukio la ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa
lililokuwa likijengwa mtaa wa Indra Ghandi, likiendelea taarifa ambazo
zilizothibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick
zinasema kuwa miili ya watu 17 wakiwamo watoto wawili mpaka sasa
imeshapatikana.Hata hivyo muda mfupi uliopita imeelezwa imeopolewa maiti
nyingine na kufanya idadi sasa kufikia 18, huku taarifa ya awali
ikisema miili ya watoto waliokolewa kwenye ajali hili iliyoacha majonzi
kwa Watanzania wakijiandaa kuisherehekea sikukuu ya Pasaka ilikuwa
wawili.
Mapema asubuhi Mkuu huyo wa mkoa
alinukuliwa kwamba miili iliyopatikana mpaka usiku wa jana ni 15 ya watu
wazima na miwili ya watoto na kwamba mmiliki wa jengo hilo na baadhi ya
wakandarasi walikuwa wametiwa mbaroni kwa ajili ya kusaidia uchunguzi
wa tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa bado juhudi
zinafanywa kutafuta miili ya watu wengine ambapo idadi ya majeruhi
waliokuwa wamenasuliwa kwenye mkasa huo walikuwa zaidi ya 20 mpaka
mapema leo asubuhi.
Taarifa zaidi zitawajia japo inaelezwa ni
vigumu kwa sasa kupatikana kwa mtu aliyehai katika kifusi kinachoendelea
kufukuliwa kwa kushirikisha vikosi vya majeshi na wasamaria wema
waliojitokeza tangu jengo hilo linalodaiwa la orofa 16 kuporomoka
asubuhi ya jana wakati watu wakiendelea na ujenzi.
No comments:
Post a Comment