Askofu Kinyunyu Dodoma, amlilia tena Askofu Laizer
ASKOFU Amoni
Kinyunyu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Dodoma, amejikuta akimlilia tena Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini
Kati Askofu Dk Thomas Olmorjor Laizer (69), baada ya kutoneshwa na Kifo
cha aliyekuwa Mzee wa Kanisa na Mwenyekiti wa Fedha Dayosisi ya KKKT
Dodoma, Lowasa Ole Sikoi.
Kinyunyu altoa masikitiko hayo Jumatatu, Machi 11th,
2013 alipohubiri katika Ibada ya kuuaga mwili wa Sikoi Chingali KKKT
tayarii kwa kuusafirisha kwenda nyumbani kwake Arusha, baada ya kufariki
kwa Shinikizo la Damu Jumamosi, Machi 9th, 2013.
Akizungumzia
pigo ambalo KKKT Dodoma imepata kwa kuagana na Marehemu Sikoi, Askofu
Kinyunyu alifananisha na KKKT ilivyopata Pigo kwa kuagana na Askofu
Laizer kutokana Jinsi Walivyolitumikia Kanisa kwa Mali zao, Muda, Akili
na Chochote walichokuwa nacho pamoja na kuwasaidia wengine.
“Wakati nikiwa
Mkuu wa Jimbo, nilimshuhudia Sikoi akilinisaidia Kanisa Dodoma kwa kila
kitu alichokuwa nacho, ambapo hata nilipokuwa naona tumekwama Jambo
fulani katika AMendeleo ya Kanisa Kirohona Kimwili, ukimuita Sikoi
alitoa Ufumbuzi wake mara moja na Jambo likafanikiwa.
“Unapotaja
KKKT Dayosisi ya Dodoma, usimtaja Sikoi utakuwa hujasema kitu, maana
hata Kiwanja cha Kanisa hili tunapomuagia sasa, kilikuwa cha kwake
lakini kwa moyo wa kulipenda Kanisa na Watu alikitoa kwa Kanisa ijengwe
Nyumba ya Kuabudia.
Hata humo
ndani wamo watu waliosaidiwa Kazi au Hali na Mali kama Kanisa
lilivyosaidiwa na Sikoi na leo hii lina na Maendeleo kama mlivyo ninyi
alivyowasaidia, hivyo msije Mkamsahau Mjane na Watoto wake! Kwa hiyo
kumbukeni wema wake na sisi Kanisa tutafanya hivyo”.alisema Askofu
Kinyunyu.
Msiba wa Sikoi
ambao ulijaa Maelfu ya watu, uliwaacha watu wakilia na kuomboleza, hasa
wakikumbuka Kazi alizolifanyia Kanisa zinazoonekana hadi leo kwa macho,
ambapo ilifika mtu mgeni anapoelekezwa au kueleza mahali aliposali kama
ni Chinangali KKKT, walizoea kusema Kanisa la Sikoi.
Aidha hadi
anafariki, Sikoi alikuwa Kiongozi na Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi
Kuu ya KKKT Dayosisi ya Dodoma, ambayo kwa miaka 22 sasa ilikuwa haina
Ofisi ya Dayosisi inayolinganishwa na Ukubwa na wingi wa Waumini nchini
na mkoani hapo.
No comments:
Post a Comment