NSSF QUEENS YAICHAPA ZSSF QUEENS 35-29 KATIKA BONANZA LA PASAKA
Kikosi cha
ZSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na NSSF
Queens katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye viwanja vya
Gymkhana mjini Zanzibar.
Mke wa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifungua
mashindano ya tamasha la Pasaka kwa timu za netiboli yaliyofanyika
katika uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar na kuzikutanisha timu za
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
wa Zanzibar (ZSSF)
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifuatilia
kwa makini mchezo wa netiboli wa tamasha la Pasaka kati ya ZSSF na NSSF
uliofanyika kswenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar. Kushoto ni
Mkurugenzi Mwendeshaji ZSSF, Abdulwakili Haji Hfidh na Kulia ni Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli na wa pili kulia ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori .
Barke Mohamed wa ZSSF (katika) akichuana na mchezaji wa NSSF Queens
Mchezaji wa NSSF, Matalena Mhagama akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa ZSSF Queens, Barke Mohamed.
Mashabiki wa
timu ya NSSF Queens wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga
ZSSF Queens 35-29 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kweye
uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.
Mke wa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Asha Seif Idd akimkabidhi ngao ya ubingwa
wa michuano ya Tamasha la Pasaka, nahodha wa timu ya NSSF Queens, Pili
Rashid Mogella baada ya kuifunga ZSSF 35-29.
Naodha
wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella akimkabidhi ngao ya ubingwa
wa tamasha la Pasaka Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa
Wateja wa NSSF, Eunice Chiume baada ya kuifunga ZSSF magoli 35-29 katika
mchezo uliofanyika katika viwanja vya Gymkana mjini Zanzibar mwishoni
mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli.
Kikosi cha timu ya NSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na ZSSF Queens. NSSF Queens ilishinda 35-29.
No comments:
Post a Comment