Friday, March 29, 2013

CHINA YATOA TATHMINI YA ZIARA YA RAIS XI JINPING NCHINI TANZANIA

Mshauri wa Utamaduni wa  Ubalozi wa  Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya  muungano wa  Tanzania Liu Dong, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu manufaa ya ujio wa Rais wa China, hali ya mkutano wa kwanza wa Bunge la umma ya 12 la China  pamoja na mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la awamu ya 12 la China. Pia China imeishukuru serikali ya Tanzania kwa mapokezi mazuri wakati wa ziara ya Rais mpya  XI Jinping ya  Jamhuri ya Watu wa China, pamoja na  waandishi wa habari katika juhudi za kuendeleza uhusiano mzuri baina ya China na Tanzania.

Mkalimali kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Jack Yu akitoa taarifa kwa wanahabari katika mkutano jijini Dar es Salaam.
 Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Liu  Dong (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ofisi za Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, kuhusu  manuafaa ya ujio wa Rais wa China, hali ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la awamu ya 12 pamoja na mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauri ya kisiasa la awamu ya 12 la China. (kushoto) ni Mkalimaki kutoka Ubalozi wa China  Jack Yu.
 Baadhi ya waandishi wa habari  wakifuatilia kwa makini taarifa iliyotolewa na Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Liu Dong. (hayupo pichani) jana katika Ubalozi wa China nchini.
Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya  muungano wa Tanzania,  LIU DONG (kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , baada ya kutoa taarifa kuhusu manufaa ya ujio wa  ziara ya Rais mpya XI Jinping Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment