Basi la Sai Baba lapoteza muelekeo na kuingia vichakani,watu watano wajeruhiwa
ABIRIA wapatao 45 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Sai
baba,kutoka Jijini Dar es salaam kwenda Masasi,mkoani
Mtwara,wamenusulika kifo,kufuatia gari yao kuacha njia na kuingia vichakani.
Tukio la ajali hiyo limetokea maeneo ya kijiji na kata ya
Mbanja,iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Katika ajali hiyo watu watano akiwemo dereva na kondakta ndiyo
waliokuwa wameumia na kukimbizwa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine kwa
matibabu.
Waliojeruhiwa ni,Juma Mtoi (Dereva),Said Mkumbwa (Kondakta) wakazi wa
Jijini Dar es salaam,na kwa upande wa abiria ni John Kasawala
(21),mkazi wa kijiji cha Nangamba,wilaya ya Nanyumbu,mkoani
Mtwara,Noel Akui (35) mkaazi wa wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na
Kuruthumu Ally (25) wakazi wa mji wa Lindi.
Said Mkumbwa ambaye ni kondakta wa basi hilo, amesema kwamba chanzo
cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele upande wa kulia kwa
dreva, ambapo liliacha njia na kutumbukia mtoni chini ya daraja la
Mbanja.
Akasema basi lake lililokuwa limebeba abiria 45 lilikuwa likitoka
Jijini Dar es salaam kuelekea wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,kufuatana
na ruti zake.
“Tulikuwa tikitokea Dar es salaam kwenda Masasi,kwani ndiyo ruti yetu
ilivyo, na ndipo tulipofika eneo hilo mpira wa tairi ya mbele upande
wa dereva likapasuka na kukosa mwelekeo kisha likagonga kingo ndogo ya
daraja na kutumbukia mtoni,,,,,,,,,tunachoshukuru ni kwamba wote
tumetoka tukiwa hao hakuna aliyepoteza maisha”Alisema Mkumbwa.
Kuruthumu Ally ambaye amepata michubuko kiasi usoni na mabegani na
John Kasawala aliyeumia kichwani,kwa nyakati tafauti walisema wao
walikuwa wamekaa sehemu ya mbele walisema wakiwa wanaendelea na safari
yao hiyo,ghafla walisikia mlio mkubwa kasha basi lao kuyumba na
kutumbukia chini ya daraja.
Akizungumza kwa niaba ya kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali
hiyo,Dkt,Edgar Mlawa amesema majeruhi hao wameumia sehemu mbalimbali
ya miili yao,ikiwemo vichwani na hali zao zinaendelea vizuri na kuna
mategemeo ya kuweza kuendelea na safari zao kama kawaida.
“Hapa Hospitalini wamefikishwa majeruhi watano tu,akiwemo
dereva,kondakta wake na abiria watatu,mmoja wao ni mwanamke, ambapo
wote hao hakuna aliyekuwa sirias kwa kuumia licha ya kupata majeraha
sehemu mbalimbali ya miili yao.ikiwa ni pamoja na vichwani”Alisema
Dkt,Mlawa.
No comments:
Post a Comment