HII HABARI YA NANCY SUMARI IMEINGIA KTK HABARI 20 BORA ZA WIKI
Stori ya Miss Africa 2005
mrembo Nancy Sumari ilishika nafasi ya tatu kwenye habari kumi bora za
jumanne march 29 2013 kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM ikiwa ni stori
iliyozungumziwa kwa dakika 4 na sekunde kumi hewani, hiyo yote ni
kutokana na uzito wa habari yenyewe ambapo pia baada ya tathmini,
imeshika nafasi ya 6 kati ya habari 20 za wiki iliyokwisha.
Kama ilikupita, ni kwamba Nancy
Sumari alizindua kitabu chake cha kwanza march 19 2013 Dar es salaam
kinachoitwa ‘Nyota Yako’ ambacho kimelenga kuwazungumzia Wanawake
wakubwa na wadogo tofautitofauti kwenye jamii na nafasi zao akiwemo Shujaa Bibi Titi Mohameda jinsi wanavyojitahidi kuleta mabadiliko na kuwahamasisha wanawake wengine kuona kwamba maendeleo yanawezekana.
Namkariri Nancy Sumari akisema
“mtoto ambae yuko shule ya msingi anaweza akamwangalia Bibi Titi na
kufananisha historia yake na akajifananisha kwa maana ya kujiamini
kutaka kufanya zaidi kwenye maisha yake na kuweza kupigania haki zake na
Wanawake wengine”
Kwenye Exclusive interview
aliyofanya na millardayo.com Nancy alijibu swali aliloulizwa kama
amehusisha historia yake ndani ya kitabu hiki ambapo alijibu “hapana
sijaandika historia yangu kwa sababu natarajia kuandika kitabu kingine
tena, yani huu ni mwanzo wa vitabu vingine vitakavyokuja kwa hiyo kwa
kuanzia nilitaka kutoa nafasi kwa Wanawake wengine ambao kuna uwezekano
tusingewasikia, nimeanza kukiandika toka mwaka jana”
Hiki kitabu kitapatikana kwenye
maduka mbalimbali ya vitabu Tanzania ambapo kingine kizuri
alichonifurahisha Nancy ni kwamba atakigawa bure kwenye maktaba
mbalimbali za shule tofauti za msingi Tanzania ili watoto wa kike wapate
nafasi ya kukisoma, sasa hivi kuna michango ya marafiki tayari
imeshatolewa ili kazi ya kuendelea kukichapisha iendelee”
No comments:
Post a Comment