Utata wa kifo kigogo UVCCM Arusha
Benson Mollel wa kwanza kushoto akiwa katika moja ya shughuli za UVCCM mkoani Arusha.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema Mollel alikutwa akiwa amekufa jana mchana na
kwamba tukio hilo limezua hofu kwa wakazi wa Jiji la Arusha, huku
wakijiuliza chanzo cha kifo chake.
Kifo cha
mwanasiasa huyo mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa madini
mkoani hapa, kimezusha maswali mengi wakati wengine wakihusisha tukio
hilo na masuala ya kisiasa na upande mwingine wakidai ni masuala la
kibiashara.
Hisia
hizo zinatokana na ukweli kwamba Arusha ni jiji lenye hekaheka za
kisiasa hasa ndani ya CCM ambapo Mollel alikuwa mmoja wa vinara wake.
Polisi
waliwasili hotelini hapo saa 8.00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu
kwenye gari na kisha kuupeleka Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya
kuhifadhiwa.
Mkuu wa
Polisi wa Wilaya wa Arusha (OCD), Gilles Muruta akizungumza katika eneo
la tukio alisema: “Tunachunguza tukio hili ambalo ni la ghafla.”
Akizungumzia
kifo hicho, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema: "Tumepokea
kwa masikitiko kifo cha Mollel japokuwa sifahamu nini hasa kimejiri
huko."
"Kuna
rafiki yake alinipigia simu kuniarifu kuhusu kifo hicho na nikawaambia
kama UVCCM Taifa tupate maelezo kamili na tujue nini cha kufanya. Iwapo
familia itakuwa na mipango yoyote watutaarifu," alisema Shigela.
Baadhi ya
wanasiasa na wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha walionekana nje ya
hoteli hiyo baada ya taarifa za kifo hicho kusambaa na wengine
walishindwa kujizuia kisha kuangua vilio.
Miongoni
mwao ni kada wa Chadema, James ole Millya na diwani wa CCM Kata ya
Mlangarini, Mathias Manga. Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Arusha,
Isaack Kadogoo ambaye pia alifika eneo hilo alisema kwamba wamepokea
taarifa za tukio hilo kwa mshtuko mkubwa.
Uongozi wa hoteli hiyo haukuwa tayari kulizungumzia kwa madai kwamba limefikishwa katika vyombo vya usalama.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya hoteli hiyo vilidai
marehemu aliwasili usiku, juzi Jumamosi hotelini hapo akiongozana na
mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nancy na kuchukua chumba namba 208.
No comments:
Post a Comment