JENGO LA GHOROFA 14 LAPOROMOKA DAR LAFUKIA WATU KADHAA
Jengo
la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa
Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na
kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi
haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha
katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka
leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama
'Tetemeko la ardhi'.
Aidha
imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa
wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza
chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza
kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote
inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji
wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali
yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Waokoaji wakiwa hoi......
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.
No comments:
Post a Comment