Saturday, September 22, 2012

Watoto wameiva katika Elimu ya Usalama barabarani Iringa

 Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Malangali, iliyopo mkoani Iringa, Steven Mligo akitoa elimu kwa watoto wenzake juu ya Usalama barabarani na namna mbalimbali za matumizi sahihi ya barabara ikiwa ni pamoja na kutambua alama mbalimbali za barabarani. Mligo alikuwa akitoa elimu hiyo katika banda la Polisi Trafiki lililopo katika maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma Kitaifa inayofanyika Mkoani Iringa katika uwanja wa Samora chinbi ya Udhamini wa Kampuni ya simu ya Airtel. 
 
Steven Mligo akitoa mafunzo kwa watoto wenzake na kuonesha dhahiri uwezo wake na jinsi alivyopata elimu hiyo ya usalama barabarani baada ya kupatiwa mafunzo shuleni kwao na maofisa wa Trafiki.
 
Mtaalam wa Elimu kutoka Mfuko wa Elimu Manispaa ya Iringa, Germana Kapinga (kulia) akimsikiliza mkazi wa mjini Iringa aliyetembelea banda lao lililopo katika maonesho ya Wiki ya nenda kwa Usalama viwanja vya Samora mjini Iringa leo.
 Wakazi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS wakijipatia bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa. 
 
Wakazi wa mjini Iringa wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Taasisi ya Usalama barabarani watu wenye Ulemavu, Getram Kabate juu ya alama mpya kuu za makundi matano ya watu wenye ulemavu za usalama barabarani.
 
Kikosi kazi ambacho leo kilikuwa kikitoa elimu ya Usalama barabarani katika Maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Iringa.
 
 Kwa lugha fasaha unaweza kumuita Fahari! Huyu dume la Ngombe ambalo linakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1000, akiwa katika maonesho ndani ya banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
 
 Wakazi mbalimbali mjini Iringa, wakiangalia Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
 
Maofisa wa Kampuni ya Airtel Tanzania wakimlisha majani dume la kisasa la Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa. Mbegu za Ng'ombe hao zinatoka Ujerumani.

No comments:

Post a Comment