Friday, September 21, 2012

AJALI ZA BARABARANI HUSABABISHWA HIVI

AJALI nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Basi hili lingine nalo lilikuwa linafanya makopsa hayo hayo ya kulipita gari lingine katika miinuka na kona kali za mlima Kitonga.
 
Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwepo RTO, SP. Pamphil Honono (kushoto) walimuona na kumsimamisha dereva wa basi hilo. Matukio haya yanatokea ndani ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. 
 
Dereva huyo alikuwa ni Issack Gerald Nyamaiswe Mkazi wa Mjini Dodoma.
  
Na hapa Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani akimwandikia Notification dereva huyo. 

No comments:

Post a Comment