Chama cha Demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) kimemuomba rais Kikwete kuwasimamisha kazi kamishna
wa upelelezi jeshi la Polisi Tanzania Paul Chagonja pamoja na kamanda wa
polisi Iringa Michael Kamuhanda kwa madai kwamba wamekua wakitoa
taarifa zisizo sahihi kuhusiana na kifo cha Daudi Mwangosi mwandishi wa
habari wa Iringa aliyeuawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa anashikiliwa na
polisi.
Mkurugenzi wa habari na uenezi
wa Chadema John Mnyika amesema makamanda hao wamekua wakitoa taarifa
zinazotofautiana na ushahidi wa picha pamoja na mashahidi waliokuwepo
kwenye tukio.
Namkariri akisema “uchunguzi
unaopaswa kuendelea unapaswa kuhusu tu ni nani hasa aliyetoa maagizo
kigogo wa juu wa polisi? lakini polisi ambao wamehusika na tukio
wanaonekana picha zao, ni askari saba walioko eneo la tukio, jeshi la
polisi limekua na kawaida ya kuwakamata raia waliopo kwenye eneo la
tukio panapotokea mauaji kwamba
ndio washukiwa wa kwanza, ni kwa nini askari wote hawa saba wanaonekana
hapa hawajakamatwa? tunataka wakamatwe mara moja kama washukiwa wakuu wa
kwanza kabisa wa mauaji, uchunguzi huru kuhusu tu ni nani alihusika
vipi kati ya hawa na vigogo gani wa jeshi la Polisi na Serikali
walihusika kuwapa maelekezo kufanya kitendo hicho cha mauaji”
Kwenye line nyingine Mnyika
amesema chama kimebaini kuwepo kwa mipango ya baadhi ya watu kutaka
kukichafulia hadhi ili kionekane ni chama chenye kusababisha vurugu na
kuwataka viongozi wote wa chama hicho kuhakikisha wanakua makini na aina
hiyo ya watu.
Amesisitiza kwa kusema
“wanakusudia kubandikiza silaha kwa hiyo tunatoa tahadhari kwa viongozi
wetu kwenye mikutano yote ya Chadema kuchukua tahadhari dhidi ya watu
wasiowafahamu ambao wengine watavalishwa mpaka mavazi ya Chadema ili
kutekeleza malengo hayo maovu” (Kwa hisani ya: millardayo.com)
No comments:
Post a Comment