Saturday, September 8, 2012

Maandamano yenyewe (picha kutoka hakingowi.com)

Zaidi ya waumini mia tatu wa dini ya kiislam jana september 7 waliandamana mpaka Wizara ya mambo ya ndani wakishinikiza jeshi la polisi kuwaachia baadhi ya viongozi wa kiislam waliokamatwa kwa kupinga zoezi la sensa.

Waumini hao walifika kwenye makao makuu wakitaka kuonana na waziri wa mambo ya ndani ili asikilize madai yao ambapo walifanikiwa kuonana nae na baada ya mazungumzo marefu kati ya serikali na waumini hao, serikali imekubali kuwaachia huru Waislamu wote waliokamatwa kupinga zoezi la sensa ya watu na makazi.

Mwandishi wa habari Masoud ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio aliripoti na namkariri akisema “ujumbe uliokwenda kuonana na viongozi wa Wizara ya mambo ya ndani umekubaliana kwamba wale waislam wote nchi nzima Bara na visiwani ambao walikua wameshikiliwa kutokana na kupinga sensa, wataachiwa huru na maandamano kuisha na hali imekua shwari, serikali imekubali kuwaachia huru”

No comments:

Post a Comment