RAIS KIKWETE AMTEUA MEJA JENERALI SAMUEL ALBERT NDOMBA KUWA MNADHIMU MKUU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ).
Mkuu
Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila
kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es
Salaam.Picha na Maktaba hivi karibuni).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).endelea kupitia audiface jackson blogspot kupata habari kila siku..Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa
iliyotolewa , Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Taarifa
hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali
Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali
Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman
A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya
kufikisha umri wa miaka 60.
Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia
Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012.
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012
No comments:
Post a Comment