AUNTY EZEKIEL’ AFUNGUKA….AMTAKA ‘NISHA’ AACHE KUJISHAUA…!!
BAADA ya msanii wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’, kulitaka Baraza la Sanaa
la Taifa ’BASATA’, kumchukulia hatua kali msanii Aunty Ezekiel kwa madai
picha zake za nusu utupu zinachafua maadili na kuwafanya wasanii wote
waonekane wahuni, naye amekuja juu na kumtaka Nisha afanye mambo yake na
aache tabia ya kumfuatilia.
Hata hivyo baada ya kutokea ishu ya Ezekiel bado wasanii wanaendelea
kukumbwa na skendo chafu kwani naye Wema Sepetu kuna baadhi ya picha
mitandaoni zinamuonesha sehemu kubwa makalio yake yakiwa wazi kitu
ambacho kinaendelea kuwamaliza bongo movie.
Ezekiel alidai kuwa haoni sababu ya Nisha, kumtolea maneno hayo kwani
hata yeye ana matatizo yake hivyo anatakiwa kujichunguza yeye ndipo
aende kwa mtu mwingine.
Alidai kwa sasa anatumia lugha ya kistaarabu zaidi yani haitaji bifu
lakini akizidi kumfuatilia atachanua makucha, ingawa hana tabia ya
kuchukuiana na mtu ila kwa hili hajakubaliana nalo kwani wapo wasanii
wagapi wanakosea na hajawahi kutoa kauli kama hiyo.
Hata hivyo aliongeza kuwa asitake kutumia kauli za mpenzi wake Ney, kuwa
makahaba wako bongo movie kwani hata mwenyewe ni mmoja wa wasanii wa
tasnia hiyo.
No comments:
Post a Comment