REDD'S MISS KINONDONI KUFANYIKA LEO, WASHINDI WA TALENT KUZAWADIWA MAPAMBO YA MWAKA MZIMA NA PERFECT LADY CLASSIC SALOON
Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye, akifungua
mashindano ya Redd's Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Sebo, ambaye
ni mmoja kati ya Viongozi wa Bodi ya waandaaji wa Redd's Miss Kinondoni
2012, ambaye alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo
lililofanyika katika hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin
Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Perfect Lady
Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar, ambao wametoa zawadi kwa
washindi watatu waliopatikana kwa kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka
mzima ndani ya Saloon yao. Shindano rasmi la kumsaka Redd's Miss
Kinondoni linatarajia kufanyika kesho katika Ukumbi wa Cassa Complex
uliopo Mikocheni, Dar.
Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.
Mshiriki namba 3, Nahma Saidi akionyesha mambo ya Pwani.
Mshiriki namba 2, Ester Musa alionyesha kipaji cha kuimba.
Mshiriki namba 1, akionyesha umahili wake wa kukata uno.
Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha jinsi ya kubuni vazi.
Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi.
Majaji wa shindano la Redd's Miss Kinondoni Talent Man Maji (kulia) na mwanadada wakifuatilia kwa makini.
Mshiriki namba 10, Kudra Lupatu akionyesha kipaji chake cha kubuni mavazi kwa staili ya kumvalisha mshiriki mwenzake.
Kudra Lupati katika pozi mara baada ya kumaliza kutambulisha vazi lake.
Mshiriki wa Redd's Miss Kinondoni akichora mlima Kilimanjaro.
Ssebo
ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012 na
alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo la Talent akimkaribisha
Mratibu wa Redd's Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa (kulia) kuongea
machache.
Mkurugenzi
wa Perfect Lady Classic Saloon, Ester Kiama ambao ndiyo waliokuwa
wamedhamini Redd's Miss Kinondoni Talent akitangaza zawadi alizowapatia
warembo walioshinda.
Wakiwa
katika nyuso za furaha ni warembo walioshinda katika Kinyang'anyiro cha
Redd's Miss Kinondoni Talent kutoka kulia ni Judith Sangu, Brigitter
Alfred na Diana Hussein. Warembo hao wamepatiwa zawadi ya kupewa huduma
Perfect Lady Saloon kwa kila mmoja kipindi cha Mwaka mzima.
Warembo wakiserebuka mara baada ya shindano hilo kuishi.
...Hapa ni mwendo wa Kwaito...
Muziki umenoga kwa mwalimu na mwanafunzi.
Ssebo
ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012 na
alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo la Talent akiongea
machache na Mkurugenzi wa Perfect Lady Saloon, Ester Kiama.
Show Love nayo ilikuwepo kwa muaandaji na mdhamini.
No comments:
Post a Comment