*TFF KUTOA VIFAA VYA SH. MILIONI 7/= HOSPITALI YA TEMEKE
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa vifaa vyenye thamani ya sh.
milioni 7.3 kwa Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambazo ni
asilimia 5 ya fedha zilizopatikana kwenye mechi ya Simba na Azam.
Mechi
hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu
mpya wa 2012/2013 ilichezwa juzi (Septemba 11 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 146, 640,000. Washabiki 26,001
walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Simba
kushinda mabao 3-2.
Sekretarieti
ya TFF inatarajia kukutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke wakati
wowote kuanzia leo ili kujua mahitaji halisi kabla ya kufanya ununuzi wa
vifaa husika.
Mgawanyo
wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 22,368,813.56, asilimia 5 ya mchango wa
kusaidia jamii (Hospitali ya Temeke) sh. 7,332,000, uwanja sh.
10,148,318.64, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
4,059,327.46, TFF sh. 10,148,318.46 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 5,074,159.32.
Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,014,831.86, kila timu sh.
32,265,025.93, asilimia 10 ya gharama za mchezo sh. 10,148,318.64, nauli
kwa waamuzi na kamishna sh. 80,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi na
kamishna 230,000, posho ya waamuzi 400,000, tiketi sh. 4,495,800,
maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na
ulinzi uwanjani sh. 2.350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh.
2,000.000.
Mchango
wa kusaidia jamii kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuzindua msimu uliopita
kati ya Yanga na Simba ulikuwa sh. 15,000,000 ambazo zilikwenda Chama
cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kusaidia uchunguzi wa kansa ya
matiti kwa akina mama.
WAKATI HUO HUO, KAMATI YA UTENDAJI IMETOA MABADILIKO YA MAREREKEBISHO YA KANUNI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana (Septemba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam imepitisha marekebisho
ya kanuni kwa ajili ya Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
Marekebisho
hayo yametokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano uliofuta Ligi ya
Taifa. Hivi sasa kutakuwa na Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya
Mkoa na Ligi ya Wilaya.
Kutokana
na marekebisho hayo ya kanuni; Ligi ya Wilaya itaendeshwa na Vyama vya
Mpira wa Miguu vya Wilaya (DFAs), Ligi ya Mkoa itaendeshwa na Vyama vya
Mpira wa Miguu vya Mikoa (RFAs).
Mechi
za mchujo (play offs) kutafuta timu zitakazopanda kwenda Ligi ya Mkoa
zitaendeshwa na RFAs wakati play offs za kupanda Ligi Daraja la Kwanza
zitakazohusisha mabingwa wa mikoa zitasimamiwa na TFF.
Ligi za madaraja yote zitachezwa mwaka mzima kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
No comments:
Post a Comment