SERIKALI KUTUMIA BILIONI 30 KUKAMILISHA UJENZI WA MKONGO WA TAIFA
Na Mwandishi Wetu, Jijini Dar
Serikali imesema itatumia shs 30 bilioni kukamilisha ujenzi wa mkongo wa taifa na kurahisisha huduma hiyo hapa nchini.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame
Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa mawasiliano
duniani (Capacity Africa) uliodhaminiwa na kampuni ya Six Telecoms ambao
umefanyika Tanzania kwa mara ya kwanza kwa siku mbili.
Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame Mbarawa |
Mbarawa
alisema ujenzi huo huko kwenye awamu ya pili huku km 7560 zikiwa
zimemalizika kuunganishwa na tayari zimeanza kutumika kwenye makao makuu
ya mikoa yote nchini na tayari kampuni sita kutoka Rwanda, mbili za
Malawi, mbili za Zambia na mbili za Burundi zimeomba kuunganishwa kwenye
mkongo wa taifa," alisema Mbarawa katika mkutano huo.
Mkutano
huo uliondaliwa na kampuni ya Six Telecoms umewakutanisha wadau wa
mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia kuitumia
Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika.
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema ujio wa mkongo
wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwenye
sekta hiyo.
Shamte
alisema lengo la mkutano huo ni kuitumia Tanzania kuwa njia ya
mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na kuongeza kwamba hiyo
itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya mawasiliano
hapa nchini.
Alisema
kuwa wamefarika sana kufanikisha mkutano huo na kutambulisha mtandao
wao wa Metro ambao unaongoza katika soko kwa hivi sasa.
Kwa
mujibu wa Shamte, pamoja na changamoto kadhaa wanazokabiliana nazo,
wameweza kujidhatiti ili kuweza kufikia lengo lao hapa nchini na katika
makampuni mengine nje ya Tanzania yanayotumia huduma yao.
“Ninafuraha
kubwa kuona mkutano huu wa Capacity Africa unafanyika hapa nchini na
mwitikio kuwa mkubwa, kwa kweli hii ni faraja sana kwetu, najua mkutano
huu utatoa picha ya nini kitafanyika ili kukabiliana na changamoto
ambazo watumiaji wa huduma zetu wanakabiliana nazo, naipongeza serikali
kwa kutoa sapoti kubwa na wadau wote duniani kukutana na hili ni kwa
ajili ya kujenga na kuleta maendeleo katika nchi zetu,” alisema Shamte.
Wadau
wa mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia
kuitumia Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika.
Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja
Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo.
Alisema
kuwa lengo la mkutano huo ni kuitumia Tanzania kuwa njia ya
mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na kuongeza kwamba hiyo
itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya mawasiliano
hapa nchini.
Wadau
wengine waliodhulia mkutano huo ni wawakilishi kutokaLiquid Telecom,
WIOCC, Safaricom Business, Seacom, Gateway na kampuni mbalimbali za
mawasiliano duniani.
No comments:
Post a Comment