Majaji usaili wa video ya Diamond watangazwa
MSANII
wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ataongoza jopo la
majaji wengine wanne kwa ajili ya kupata wasichana na wavulana watakaoshiriki
kwenye video yake mpya.
Usaili
wa watu hao utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, mjini Dar es
Salaam ambao wote watakaochaguliwa kuonekana kwenye video hiyo itakayorekodiwa
na kampuni ya I-View Studios watalipwa.
Katika
orodha hiyo, yupo mbunifu wa mitindo wa kimataifa, Ally Rehmtullah ambaye hivi
karibuni alizindua mavazi yake mapya katika hoteli ya Serena, yupo pia Raqey
Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios,pia Creative
Director, Sammy Cool ambaye ni mwalimu wa dansi na blogger maarufu Missie
Popular.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter
Mwendapole alisema majaji hao wamechaguliwa kutokana na kuhusika kwao na
shughuli za sanaa kila siku.
“Diamond
ndiye mwenye video na ni mwanamuziki, Raqey ndiye atakayerekodi video, lazima
ajue watu ambao ana wataka kwenye hiyo video, ameshafanya kazi kama hizi mara
nyingi, ni mpiga picha wa kimataifa, Sammy Cool ni densa maarufu na mwalimu
ambaye amewafundisha watu wengi katika ulimwengu wa kucheza nchini, wengi
watakuwa wakimfahamu tangu enzi za Bombeso, THT na mashindano mbalimbali ya
urembo, amekuwa pia akitoa ushauri nasaha.
“Kwa
upande wa Ally ni mbunifu wa mitindo wa kimataifa, ameshafanya kazi mpaka
ulaya, ana uzoefu mkubwa kutokana na kazi zake kwa hiyo kuwepo kwake kutasaidia
pia vipaji vingine kuonekana, Missie Popular yeye ni mwandishi, mwanamitindo
kwa hiyo kama mtu wa habari ana mchango wake katika kuibua vipaji pia,”
amesema.
Mwendapole
amesema usaili huo utaanza saa tano kamili asubuhi na kwamba baada ya usahili
huo wale watakaochaguliwa watafahamishwa mazoezi yatakuwa wapi na baada ya hapo
kazi ya kurekodi video hiyo kuanza.
Video
hiyo ambayo wote watakaochaguliwa kuonekana watalipwa, itarekodiwa maeneo
mbalimbali nchini pamoja na sehemu nyingine nje ya bara la Afrika ili kuipa
ladha tofauti. Kampuni ya I-View ndio imeshinda mchakato wa kurekodi video
hiyo.
Tayari
kampuni hiyo imeweza kutengeneza video kadhaa za kiwango cha kimataifa ikiwemo
Kwasakwasa Tazneem, Utanikumbuka ya Suma Lee pamoja na matangazo mbalimbali ya
biashara. I-View pia ndiyo inatengeneza kava za wasanii mbalimbali Bongo Movie
ambao wanafanya kazi na Steps Entertainment.
No comments:
Post a Comment