Monday, April 1, 2013

UPDATE: WALIOFUKIWA NA KIFUSI KWENYE MGODI WA MORAM JIJINI ARUSHA YAFIKIA 20

WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga aina ya Moramu katika machimbo yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.

Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .

Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.

Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.

No comments:

Post a Comment