Thursday, November 1, 2012

ZAIDI YA WANAKIJIJI 600 WAPEWA HUDUMA YA AFYA MONDULI.

Dk.Song Gmhwa(kulia) raia wa Korea akimwangalia Bibi wa kimasai, Naniai Poranda, macho kwa kutumia kifaa maalum ambayo yanamatatizo ya kuona wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu.
 Dk.Song Gmhwa(kulia) raia wa Korea akimwangalia Bibi wa kimasai, Naniai Poranda, kinywa kwa kutumia kifaa maalum  wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu
 Dk. Seung Woo Park(kulia) raia wa Korea  akimpima Bibi wa kimasai,Ngaisi Sumuni wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu.
Dk.Moon Eunmi (kushoto) raia wa Korea akimwelekeza Mama wa kimasai,Nariku Ngera namna ya kutumia dawa kwa kumpa Mtoto wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu

Wanakijiji zaidi ya 6000 wanaoishi katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wamepata huduma ya afya ikiwa ni pamoja na upimaji wa magonjwa mbalimbali sanjari na utowaji wa madawa.

Zoezi hilo ambalo linaendeshwa na Kampuni ya Samsung kupitia wafanyakazi wake Samsung Medical Center na Samsung electronics kwa kujitolea wakishirikiana na shirika la Chakula kwa ajili ya Majanga la Korea(KHFI)  wanaendesha zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali pamoja na utowaji wa madawa kwa wanakijiji hao. 

Meneja wa Kampuni ya Samsung kwa Afrika mashariki Bw.Makunga Mugo nalisema kuwa wafanyakazi kutoka katika kampuni hiyo wanajitolea katika kuwasaidia wananchi mbalimba wenye mahitaji kwa Afrika nzima na sasa wako Tanzania Mkoani Arusha.
Alisema kuwa wamejikita zaidi kwa vijana huku akidai kuwa wao ndio nguvu kazi katika kila nchi kwani wanaamini wakimuwezesha kijana wamewezesha jamii nzima inayomzunguka.

Naye diwani wa kata ya Elmorijo Bw.Bariki Sumuni alisema kuwa anatoa shukrani kwa wafadhi hao kwa kuwa wamejaribu kuokoa maisha ya wazee,wamama,vijana na watoto kwa kutoa huduma ya vipimo pamoja na utowaji wa madawa bure jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa katika kijiji hicho.

Alisema kuwa huduma ya Afya ipo umbali kwa kilometa 12 hadi kufikia katika zahanati ya kijiji hali ambayo imekuwa ikiwapa shida hasa kwa kinamama wajawazito wakati wa cliniki na wakati wa kujifungua.

Aidha alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa maji kijiji hapo kutokana na eneo hilo kuwa katika muinuko wa juu kama panavyojulikana kwa jina la Monduli juu.

“Kampuni ya Samsung imetusaidia sana hapa kijijini hata imetujengea shule na pia nimezungumza nao wamenihaidi kuwa watajenga zahanati hapa kwakuwa tayari kunampango wa kuwa na kijiji kipya kutokana na ongezeko la watu”alisema Sumuni
Kwa upande wake mfanyakazi KHFI na Korea charch mission  Bw.Daniel Vayani alisema kuwa wametenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwaajili ya ukarabati wa shule pamoja na kuwasomesha bure watoto wanaoshi katika mazingira magumu
Alisema kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni pamoja na kuwepo kwa muamko mdogo wa elimu katika mila,watoto kukatisha masomo.

Mmoja wa wagonjwa aliyepatiwa matibabu ya bure katika zoezi hilo Bi.Maria Devid (60)alisema kuwa yeye alifanyiwa upimaji katika baadhi ya mwili wake ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa,macho na kutosikia vizuri 

“Kweli nawashukuru sana hawa wafadhili Mungu awabariki kwa kuja kutupa hii huduma ya bure ,zahanati yetu ya kijiji ipo mbali hivyo leo tumepata fursa nzuri sana”alisema
Katika zoezi hilo pia upimaji wa magonjwa mbalimbali unafanyika na upimaji huo unawashirikisha wazee,vijana,wanafunzi pamoja na watoto wadogo ambapo zoezi hilo litadumu kwa siku mbili.

No comments:

Post a Comment