Mashabiki wa Simba novemba 5, 2012 waliandamana mpaka kwenye makao makuu ya club hiyo Msimbazi
Kariakoo Dar es salaam wakiwa na mabango mbalimbali yanayomaanisha
wamechoka na ishu mbalimbali za club hiyo.
Mabango mengine yalisomeka
kwamba mamluki wajirekebishe Simba mmeikuta, mengine Ndugu Kaburu kocha
wetu Milovan mchango wake mkubwa bado tunamuhitaji, Kaseja tuachie timu
yetu.
Hiyo yote imetokana na Simba kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar novemba 4 2012 Morogoro.
BAADA ya kichapo hicho msimamo
wa ligi kwa timu kongwe jijini Dar es Salaam, YANGA SC imepanda kileleni
mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Azam FC mabao
2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga
iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya
mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na
Simba SC yenye pointi 23, ambayo imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini
Morogoro.
Mchezaji wa zamani wa Ghana na
klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa, Abedi Pele, leo ni siku ya
birthday yake ametimiza miaka (48).
Mchezaji huyo amekuja nchini kufanya ziara ya kuangalia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ya soka la Tanzania.
Pele, ambaye aliiongoza
Marseille kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya mabao
dhidi ya AC Milan ya Italia mwenye watoto wawili wanaocheza mpira ambao
ni Jodan na Dede wanachezea Olimpic Marseille ya Ufaransa.
No comments:
Post a Comment