HII NI KALI KULIKO; ANGALIA PICHA YA MAGARI ZENYE UWEZO ZA KUPAA ANGANI NA KUTEMBEA BARABARANI
Hili ni Moja ya Magari hayo ambalo likitua tuu hapa linakuwa gari la kawaida
Hili lipo hapa linakaribia kuondoka
Hapa Gari Hilo likiwa Juu linakula mitaa
Muda mchache baada ya kutua sasa lipo mtaani linatembea,
Foleni Ikizidi Hiloo lina tambaa juu
Hii ni Aina nyengine ya Magari hayo ambayo hupaa na kutembea nchi kavu
Cheki Hapa limetua kwa kasi mwendo Mdundo linaendelea na safari
Hili ni aina ya Gari ambalo pia Hupaa na kutembea Barabarani
Hapa Kabla halija ondoka , Limekula pozi
Hapa linakula Kona.
Kutokana
na kukuwa wa mabadiriko ya Science na Technology kumekuwa na mambo
mengi sana ambayo yanatokea, lakini kubwa kabisa la siku ya leo ni ujio
wa haya magari ambayo wanasayansi wanatarajia kuyazindua hivi karibuni,
mpaka sasa yapo katika majaribio kabla ya kuanza kutumika Rasmi.
Wazo
hili la kutengeneza magari haya yenye uwezo wa kutembea katika barabara
za kawaida na kupaa angani limekuja kutoka Holy hood, ambapo
wanasayansi hao walifanya utafiti kwa lengo la kutengeneza magari haya
kama Taxii za mwendo kasi ili kurahisisha safari za abiria wenye haraka
zao, Lakini kwa mara ya kwanza mpango huo ulikwama kutokana na kwamba
walikuwa hawajajiandaa, waliweka zaidi kama mpango wa kusadikika.
Baada
ya ya muda kupita waliweza kufanikiwa na mpango huo wa magari ambayo
yanaweza kupaa angani endapo tuu kutakuwa na foleni kubwa hasa kwa nchi
za Ulaya na Marekani.
Kwa
hakika magari hayo ambayo ni Technology mpya kabisa Hapa duniani ni ya
kipekee na ambayo itawafanya watu wapate kuishi kwa amani kabisa.
Akizungumza mmoja wa wagunduzi wa Magari hayo yaliyo pewa jina la
"SKYWORTHY" amesema kuwa " Tumelazimika kutafuta ufumbuzi wa kupunguza
msongamano wa foleni na kuwasaidia wenye haraka pindi wakiwa na haraka
waweze kupaa moja kwa moja na kuwahi mambo yao"
Pia
katika haya magari jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba mbawa zake
zimetengenezwa kiasi kwamba huwezi kuziona wakati Gari lipo barabarani,
lakini wakati linaanza kupaa ndipo mbawa hizo zinatokezea, hilo ni swala
ambalo wanasayansi hao wameonesha ubunifu mkubwa sana na wakipekee,
swala ambalo halijawahi kutokea hapo mwanzo.
Magari
hayo ambayo pia ni Ndege yanatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu 2012 ambapo
gari la kwanza litauzwa kwa Gharama ya Dola za Kimarekani 300,000,
ambapo ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kupaa kwa masaa 20 angani.
Magari
hayo ambayo pia ni ndege hapo hapo yana muundo wa Chopa , lakini ni
ndogo zaidi ya Chopa, ina uwezo wa kukimbia (110mph/180 km/h) ambayo ni
sawa na (560km/350Miles)