Stori za uhakika nilizozipata
muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambaye alikuwa
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy
Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012.
Oktoba 23 2012 Kamanda wa
polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwa akisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes
tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30
pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo
mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama
Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia kwenye maeneo
ambayo kunakuwa na harusi, sehemu ambazo kunakuwa na magari mengi watu
hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia
kwa makosa ya wizi”
No comments:
Post a Comment