STORY YA KUSISIMUA; SIMULIZI YA KAHABA
Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini
dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa
bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na
bosi wangu .
Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na
kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa
, hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na
kunijali kila kitu nilipata na zaidi .
Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na
watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea
nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo .
Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi
mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja
mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani
ameshanifia
Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku
nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa , nilimwamini
sana nay eye aliniamini sana , miezi 3 tokea kujuana na huyu kijana
aliniambia kuhusu kufanya nae tendo la ndoa .
Nilifikiria sana wakati mwingine nilitaka kulia
jinsi alivyokuwa ananishika na kuniomba tendo la ndoa akiwa chumbani
kwangu , alijaribu kunishika sehemu kadhaa akanivua nguo nami nilimtolea
nje nilimkatalia .
Basi siku moja nikamwomba tukaangalie afya zetu ,
kijana wa watu alikasirika sana wiki nzima hakufika nyumbani kwangu wala
kunipigia simu , kumbe alitaka tufanye tendo la ndoa bila kinga ? sasa
ningejuaje kuhusu afya yake ? au ananiamini nini mimi ?
Maisha yaliendelea na mambo mengine yaliendelea tu
wiki ya 3 alinipigia simu akaniomba msamaha turudiane na alikubali
kwenda na mimi kupata vipimo vya afya zetu kujua kwanza kabla hatujaanza
mambo mengine yoyote yale .
Basi ndio hivyo majibu yaliyoka mazuri , ndio
mapenzi yetu alikuwa zaidi na penzi nilimpa bila hiyana wala aibu yoyote
, yeye mwenyewe alifurahia mambo yangu na kwanza alikuwa anatoroka
nyumbani kwao kuja kulala kwangu wakati mwingine mwezi mzima .
Tuliendelea kwa miezi kadha na huyu kijana huku na
mimi nikiwa na bosi wangu kule kazini , basi bwana siku moja , sisi
officini tulitakiwa kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika
maadhimisho ya siku ya afya duniani . Watu walipimwa afya zao na mimi
nilipimwa , majibu yangu yalikuwa ya kutatanisha sikuamini macho yangu
wala masikio yangu , nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale
yale kwamba nimeadhirika na UKIMWI .
Haya majibu yalimfikia mpaka bosi wangu nae
akatambua hilo akasikitika sana nay eye alivyoenda kupimwa akakutwa
hajaadhirika , basi nikajua moja kwa moja ukimwi nimepata kutoka kwa
yule kijana wa mitaani na sio mtu mwingine .
Nikamwomba huyu kijana tukaangalie afya zetu kwa
mara ingine tena hospitali , tukaenda kule kupima afya zetu , yeye ndio
alikuwa wa kwanza kupokea majibu yake , alikutwa ameadhirika akupata
mshituko wa ghafla yaani haamini .
Mshituko huo ulimpelekea aanguke chini na kuzimia
watu walienda kumbeba na kumpeleka hospitali kupatiwa huduma ya kwanza
basi hapo ndio magonjwa mengine yalianza kujitokeza na kujulikana sana .
Kumbe huyu kijana alikuwa na urafiki wa kimapenzi na
shugamami mmoja mtaa wa pili huyu shuga mami mume wake alifariki dunia
miaka 5 iliyopita kwa UKIMWI watu wanaema TB sijui , ndio huyu kijana
kuona zile pesa za shuga mamy akaenda kwake .
Kijana aliumwa kwa miezi 3 hivi kisha akafariki
dunia akaniacha duniani mwenyewe , kule kazini nilifukuzwa kaza na bosi
wangu kisa nilitaka kumwambukiza ugonjwa wa ukimwi , lakini siku moja
alinipigia simu kunieleza kwamba mke wake ameadhirika na UKIMWI pia
lakini yeye anasema hajaadhirika .
Hapo ndio nilishangaa sana , kwanini mke wa
aadhirike yeye asiadhirike au mke wake nae alikuwa anatoka nje ya ndoa
bila mume wake kujua ? basi hiyo ni siri yao nyumbani kwao mimi
hayanihusu .
Lakini ndio hivyo nilikuwa nimeshaadhirika na UKIMWI
kazi nimeshafukuzwa sina cha kufanya wala kutafakari nilifikiria zaidi
kuhusu ugonjwa wangu wa UKIMWI na jinsi nitakavyoweza kuishi maisha
marefu kwa matumaini .
KAHABA
Baada ya kuona maisha magumu na sina lolote la
kufanya mimi kama mwanamke mrembo na mwenye mvuto niliamua kutafuta njia
rahisi zaidi ya kujipatia kipitano nilifikiria njia nyingi sana ambazo
zingeweza kunipatia angalau mlo na mavazi katika siku zangu za maisha
zilizobakia baada ya kugundulika nina virusi vya ukimwi
Nikaanza kutafuta sehemu ambazo naweza kuuza mwili
wangu kwa pesa za chapchap niweze kuendeleza maisha yangu ya kila siku ,
nilikuwa na ramani yangu kwanza pale OHIO , JOLLY , MACHENI , BILLS NA
LATAVERNA hizo ni sehemu 5 kuu za starehe jijini dare s salaam kwahiyo
huko naweza kufanya kazi za kujiuza kwa wiki nzima kila siku bila
kuchoka .
Ohio ilikuwa nzuri ila tatizo lake ni kwamba kila
anayepita pale anakujua halafu unatakiwa uonyeshe maungo yako hazarani
mimi sikuzoea tabia hizo na sikuwa na mhemko huo kwahiyo nilivaa miwani
yangu na kuacha mapaja nje tu waangalie wenyewe kama wanapenda watakuja .
Kule macheni tatizo lake ni mashoga wengi sana , yaani mwanaume anaweza
akaja kutafuta Malaya akakuchanganya wewe ni shoga , wale mashoga
wanaojiuza hawana tofauti na sisi wanawake tunaojiuza wakati Fulani
ulitokea ugomvi mkubwa watu waliamulia tulimgombea mwanaume .
Billa nako kuzuri ila vijana wengi sana halafu
hawana pesa , na vitoto vidogo vingi , nilikuwa naogopa matatizo na
vijana wa kule sikupenda kufanya mchezo na watoto wadogo waliokuwa
wananitaka hata kwa dau gani nilingoja wanaume wenye pesa zao tu sio
zaidi .
Basi nilianza safari za kuelekea jolly club kwa
ajili ya kujiuza mwili wangu nipate angalau chochote cha kula na kufanya
katika maisha yangu , pale jolly club nilikutana na dada mmoja anaitwa
Aisha , huyu dada nae ni kahaba mzoefu akaanza kunionyesha mambo kadhaa
wa kadha kuhusu biashara ya ukahaba na kadhalika . Hapa ndio nilijufunza
kwamba sio makahaba wote ni masikini au hawajiwezi kuna wengine
wanajiweza na wanazo fedha ila wanapenda kufanya ukahaba yaani wamechoka
na dunia wengine walikuwa na wanaume wao wakaachika wakaamua kuja huku
kwenda na mwanaume wowote yule anayekuja .
Wengine wana matatizo katika ndoa zao kupigwa na
kadhalika wanaamua kuja huku kujiuza au kukaa huku ili kuepuka matatizo
katika ndoa zao au mahusiano yao , wengine ndio kama hivyo waume zao
hawana nguvu za kutosha kufanya nao tendo la ndoa wanaamua kuwa makahaba
kila mtu na lake na mambo yake pia .
Wengine wanafanya huu ukabaha kwa ajili ya
kupeleleza yaani ni wapelelezi wa polisi au watu Fulani katika serikali
wako katika mitaa hii kuzuga tu , ili wafanikishe kazi zao za uchunguzi
kama polisi wa usalama sehemu walizoko .
Mwisho wa yote siku hizi kuna vita kubwa katika
biashara hii ya ukabaha mjini dare s salaam , mfano kule jolly kuna
wazungu na wahindi wanakuja kufanya biashara ya ukahaba kwahiyo wewe
mwamfrika unakazi ngumu kuwapita wale wazungu na wahindi au wachina .
Siku hizi wanaume wengi wanapenda kitu kinaitwa
JICHO yaani kufanya mapenzi kinyume na maumbile , hii nayo ni soko kuu ,
mfano mwingine anaweza kuja kwako anataka jicho na wewe hutoi jicho
maana yake unakosa soko suluhicho ni kujitoa mhanga na kufanya mapenzi
kwa kuwa mteja ni mfalme .
Mbaya zaidi kuna wanaume wengine wanakuja wanaweza
kukuchukua uende nao kufanya ngono kumbe wanakupiga filamu za ngono
wakati unafanya kitendo hicho haswa wazungu wengine wanakupa ufanye
mapenzi na mbwa wao au wanyama wao wengine mambo yanaenda hivyo .
Biashata hii ya ukahaba ilinichanganyia sana kwa
miaka 2 niliyoifanya na kwa kweli hakuna aliyenijua kama nimeadhirika na
ugonjwa wa ukimwi nilikuwa najitunza na kutuza siri zangu hizi kuu na
sikupenda kuzoeana na watu sana hadi waniulize hivyo
Siwezi kuhesabu ni watu wangapi nimefanya nao ngono
lakini ni zaidi ya 300 siku zingine nafanya kazi na watu zaidi ya 3 kwa
siku moja kwahiyo mambo yanaendelea halafu wengi hawakupenda kutumia
mipira ya kiume yaani kondo walipenda kuja hivi hivi tu bila kinga
chochote kile
Na mimi nilikuwa nimeshaadhirika nilichokuwa
natafuta ni fedha za kuendeleza maisha yangu kwahiyo hata kama nikifanya
ngono zembe bila kinga mimi hainiumi sana kwa kuwwa nilishajua hali
yangu sikuweza kuitengua siku wa chochote cha kufanya zaidi ya hichi .
Hii ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa maasi ambayo yule
kijana alinifanyia kuniambukiza UKIMWI kwa makusudi huku akijua kabisa
ameadhirika siku nyingi ,kwakuwa yeye ameamua kuniuwa mimi basi na mimi
nauwa wengi zaidi na sijali kuhusu dhambi hizi nilizozifanya na sijutii
kabisa .
MAISHA YA MTAANI
Huku mitaani waliniita majina kama JLo wakati
mwingine salma hayek yaani wale waigizaji maarufu duniani kwa urembo
nilio nao na mvuto wake , hakuna hata mmoja aliyekuwa na mawazo kama
nimeadhirika au la kwa maana yule kijana niliyekuwa nae kama mpenzi
alikufa kifo cha ghafla watu walisema amekufa kwa pressure .
Mitaani napo nilikamua kinoma , waume za watu
walikuja mpaka mlangoni kwangu na magari yao , wananipakia na kunipeleka
katika kumbi za starehe na sehemu nyingine nyingi sana wengine
walinihonga mali na mambo kibao kisa wamenipenda wanataka ngono
Na kwa uhakika hawa wanaume niliwapanga sawia kabisa
na hakuna aliyeweza kutambua mimi nina wanaume wangapi na wanaishi wapi
wengi walijua ni washirika wangu katika kazi zangu na mambo yangu
mengine kwanza sikupenda kuongea na mwanaume wowote chumbani kwangu wote
nilikuwa nawaambia tukutane mbali kidogo na nyumbani haswa kati katika
ya jiji .
Katika hawa wateja wangu kulikuwa na kijana mmoja
anayeitwa juma huyu juma alikuwa na rafiki yake mmoja anayeitwa Shy ,
kijana mwembamba mwenye umbo la wastani , hana ndevu halafu ni mcheshi
sana , alifanikiwa kuiteka moyo wangu , sasa nilitaka kumwambia mara
kibao kwamba nimemzimia
Tatizo ni kwamba anayekuja kunichukuwa pale ni juma ,
juma huja pale kwa kusindikizwa na Shy , basi juma akanitambulisha
katika website moja inayoitwa darhotwire www.darhotwire.com , nyumbani
nikienda kupumzika nilipenda kushinda katika tovuti hii kuchat na
marafiki na watu wengine .
Huyu shy nae nilimkuta katika site hii usiku wa
manane anachat na jamaa zake , ila siku moja nilikutana na kijana
mwingine anayeitwa politeman , huyu ndio alinichanganya kabisa , kwanza
jina lake na jinsi aliyokuwa anaongea kweli nilizimia mwenyewe bado
nikawa na siri kubwa moyoni je hivi tukifanya ngono inakuwaje ?
Maisha yaliendelea tu , basi nikimpenda politeman ,
huyu kijana akawa anakuja mpaka nyumbani kwangu wakati mwingine na huwa
nampa computer yangu aitumie tukaenda zaidi nilimshitukia kumbe huyu
polite ana urafiki wa kimapenzi na dada mwingine anayeitwa salma siku
moja walipanga kwenda kufanya mapenzi lakini polite akakataa ?
Sikuamini macho yangu wala masikio siku nyingi kama
naota kumbe polite alikuwa na urafiki na dada mmoja anaitwa Maria Chipz
?? Sikuamini , nilimuheshimu sana maria na sikutegemea kama anaweza
kufanya hivyo hata siku moja , muda ukaenda kumbe kuna dada mwingine
anaitwa REHEMA naye alikuwa anampenda Politeman Miss upanga Naye
anampenda Politeman we acha tu
Nikamwaga chini sikupenda tabia zake za kitoto
kitoto anazowafanyia hao kina dada wengine ingawa nilifanya nae mapenzi
kama mara 4 hivi na mara zote hatukutumia kinga na nilikuwa nimeadhirika
ila ni siri yangu , polite hajui na wengine wote hawajui lakini ndio
maisha hayo
Haya ndio hivyo , nami sasa hivi nakaribia kufariki
dunia niko zangu kitandani hapa hospitali ya Amana mkoani dar es salaam ,
kweli maisha ni safari ishi upendavyo na sio watakavyo , mwisho wa yote
dunia sio hadaa wala dunia haikuchukii au haitaki kukufanyia chochote
kibaya
Bali watu ndio hadaa , hata kama ni ndugu yako
rafiki yako , hakikisha humpi nafasi akutawale aweze kukumiliki wewe na
kukuamrisha chochote kile anachotaka yeye , kama ukifanya hivyo ndio
utaishia kubaya kama mimi
Bosi wangu alinimiliki sana nikampa penzi , kijana wa mitaani nae alinimiliki mpaka sasa nimeaona faida zake na hasara zake
Wacha ningoje siku zangu nife nizikwe niende ahera Kwaheri .
😢
ReplyDeleteRip
ReplyDeleteNice story
ReplyDelete