ALIYEMUIBIA HAKIMU SINGIDA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU.
Jengo la mahakama ya mwanzo Utemini mjini Singida.
Mlinzi
wa kibanda cha biashara cha hakimu wa mahakama ya mwanzo Ipembe mjini
Singida Jumanne Juma (47), amehukumiwa kutumikia jela jumla ya miaka
minne na miezi sita, baada ya kukiri kutenda makosa matatu likiwemo la
kuvunja kibanda cha mwajiri wake kwa lengo la kufanya uhalifu.
Mlinzi Jumanne anatuhumiwa kutenda makosa hayo,Novemba 3 mwaka huu saa tano usiku eneo la Utemini mjini Singida.
Mshitakiwa
Jumanne ambaye ni mlemavu wa jicho moja la kushoto (chogo), aliajiriwa
na hakimu Hossea Selema Mkude (58) wa mahakama ya mwanzo Ipembe.
Katika
shitaka la kwanza, mshitakiwa alisomewa kuwa mnamo Novemba 23 mwaka huu
saa tano usiku huko Utemini, mshitakiwa bila halali, alivunja kibanda
cha mwajiri wake kwa nia la kutenda kosa la jinai.
Shitaka
la pili, mshitakiwa Jumanne alisomewa kuwa katika siku ile ile na
wakati huo huo ,aliiba mizani ya kupimia uzito na vocha mbalimbali za
simu za viganjani, vyote thamani yake ni shilingi laki tano (500,000).
Aidha,
ilidaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa hakimu Mkude, alipuuza na
hivyo akishindwa kuzuia kosa la wizi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Mshitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yake hayo, bila kuuma uma mdomo, alikiri kutenda makosa hayo.
“Kwa
hiyo, naiomba mahakama yako tukufu, inionee huruma kwa vile sijasumbua
kabisa nimenyoosha maelezo yangu moja kwa moja, pia nipo tayari kumlipa
Mheshimiwa wangu Mkude sh.500,000 anazodai kuibiwa”, alisema mshitakiwa
Jumanne huku akiinamisha kichwa chake chini.
Kwa
upande wake hakimu wa mahakama ya Utemini Ferdnard Njau, alisema pamoja
na maombi ya mshitakiwa, mahakama ipo pamoja na mambo mengine,
kurekebisha tabia mbaya zinazofanywa na baadhi ya watu.
”Kwa
kosa la kwanza, utatumikia jela miaka mitatu, kosa la pili, miezi 12 na
kosa la tatu, miezi sita. Adhabu zote zitakwenda pamoja na hivyo
utatumikia jela miaka mitatu tu”,alisema hakimu Njau.
No comments:
Post a Comment