SIMBA NA LIGI KUU:
Simba ambao ni mabingwa
watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wameendelea kuokota pointi moja moja
katika michezo ya nje ya Dar es salaam baada ya october 31 2012
kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mechi na Polisi Morogoro ambao
wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.
Kutokana na matokeo hayo Simba
na Yanga wana pointi 23 kila mmoja sasa hivi hivyo wanatofautiana kwa
magoli ya kufunga na kufungwa huku kila timu ikiwa imeingia uwanjani
mara 11.
IDADI YA VITUO VYA MAFUTA VINAVYOFANYA KAZI MBEYA KWA SASA KUTOKANA NA UHABA.
Mwandishi wa habari Joseph
Mwaisango kutoka Mbeya ameripoti kwamba upatikanaji wa mafuta kwa siku
hizi mbili tatu 87.8 umekua wa tabu, ni vituo vitatu tu vya kuuza mafuta
vinavyouza mafuta kwa sasa ambavyo ni kwa Mama John, Mwanjelwa na
katikati ya Forest mpya ambapo kuna foleni kubwa sana, bei ya mafuta ni
ileile isipokua walanguzi ndio wanauza lita moja kwa elfu 5.
MOJAWAPO YA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUZUIA AJALI ZA MAJINI.
Kutoka bungeni Dodoma 104.4 ni
kwamba Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe amesema Serikali
imechukua hatua kadhaa kuzuia ajali za kwenye maji ambazo zimepoteza
maisha ya watanzania wengi kwenye ajali zilizopita ambapo mawapo ya hizo
hatua ni kuacha kusajili meli zenye umri wa zaidi ya miaka 15.
Pia Serikali imeahidi
kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya utafutaji na uokoaji wa majini
na angani ili kuhakikisha shughuli za uokoaji zinafanyika kwa kuzingatia
sheria wakati ajali zinapotokea.
No comments:
Post a Comment