Saturday, December 22, 2012

YAYA TOURE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA, ZAMBIA TIMU BORA, KIKOSI CHA AFRIKA SUNZU NDANI


ACCRA, Ghana
KIUNGO Yaya Toure wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City inayoshikilia ubingwa wa England ametwaa kwa mara ya pili mfululizo Tuzo ya CAF ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2012.
Yaya alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo wakati wa sherehe za ugawaji tuzo zilizofanyika jijini Accra usiku huu (Desemba 21, 2012) kwenye ukumbi wa Banquet, ikulu mjini Accra.
Kura hizo zilipigwa na makocha wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa mashirikisho ya soka yanayotambuliwa na CAF.
Waziri wa Michezo wa Ghana, Clement Kofi Humado na Waziri wa Habari, Haruna Iddrisu ndiyo waliokuwa wageni wa heshima katika hafla hiyo, kama ilivyokuwa kwa rais wa CAF, Issa Hayatou na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Ushindi huo wa tuzo mara mbili mfululizo unamfanya Yaya (29) kuwa katika kundi moja na El- Hadji Diouf wa Senegal na Mcameroon Samuel Eto’o ambao pia waliwahi kuweka rekodi hiyo. 
Drogba ambaye shuti lake la mwisho katika hatua ya "matuta" liliisaidia Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na pia akafunga goli jingine lililoisaidia Chelsea kutwaa Kombe la FA, alizidiwa na Toure aliyeisaidia Manchester City kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu ya England walilolikosa kwa miaka 44 .
Hii ilikuwa ni mara ya nne pia kwa sherehe za ugawaji wa tuzo hizo kufanyika nhini Ghana, miaka mingine ikiwa ni 2006, 2009 na 2011.
ORODHA YA WASHINDI 2012 NA ZAWADI ZAO:
Mwanasoka Bora wa Afrika                  – Yaya Toure (Ivory Coast)
Mwanasoka Bora anayecheza ndani     – Mohamed Aboutrika (Misri)
Tuzo ya Nidhamu                                  -- Timu ya taifa ya Gabon
Kocha wa Bora wa Mwaka                   – Herve Renard
Timu Bora ya Taifa:                              -- Zambia
Timu Bora ya Taifa ya Wanawake   -- Equatorial Guinea
Klabu Bora ya Mwaka                      –  Al Ahly (Misri)
Refa Bora wa Mwaka                        – aimoudi Djamel (Algeria)
Yosso mwenye kipaji                           --  Mohamed Salah (Misri)
Mwanasoka Bora wa kike                 – Genoveva Anoman (Equatorial Guinea)
Tuzo ya Gwiji                                      -- Mahmoud El-Gohary (Misri)
Tuzo ya Gwiji                                    --   Rigobert Song (Cameroon)
Tuzo ya Platinum                               -- John Mahama (Rais wa Ghana)
KIKOSI BORA CHA NYOTA 11 WA AFRIKA (XI) 2012:

Kipa: 
Lutunu Dule ( kongo)
Mabeki:  
Ahmed El- Basha (Sudan), Walid Hicheri (Tunisia), Stoppila Sunzu (Zambia) na Ahmed Fathi Misri)
Viungo: 
Mohamed Aboutreika (Misri), Yaya Toure (Ivory Coast), Alex Song (Cameroon), Younes Belhanda (Morocco)
Washambuliaji:  
Didier Drogba,(Ivory Coast) na Christopher Katongo (Zambia)
Kocha: 
Herve Renard (Ufaransa)

No comments:

Post a Comment