Ni DMM 88.5 yani Dar mpaka Moro
huku 88.5 ikiwa ni namba rasmi kwa kila mwanafamilia wa CLOUDS FM Dar
es salaam na Morogoro ambapo CLOUDS FM licha ya kuwa imeandaa party ya
kwanza ya aina yake inayoanzia kwenye treni mpaka bush party, kwa mujibu
wa TAZARA hii inakua party ya kwanza na ya kipekee kwenye historia ya
Tanzania.
Ni bata kwenda, bata kufika na
bata kurudi ambapo Watanzania waliovutiwa kujiunga nasi kwa pamoja
tunaenjoy kwenye miaka 13 ya kuzaliwa kwa CLOUDS FM lakini pia
kusherehekea ujio wa kamanda mpya wa 88.5 Dar es salaam baada ya
kumaliza mkataba wa 88.4 kwa kipindi cha miaka 13.
Safari itaanza asubuhi december 28 2012 saa mbili kamili pale
TAZARA na tutatumia saa nne njiani tukiwa kwenye treni huku tukipita
kwenye vivutio mbalimbali vya Tanzania kama mbuga ya wanyama ya Seluu na
kwenye chemchem inayotoa maji ya moto.
Kwenye treni kutakua na huduma ya chakula na vinywaji ambavyo
vitakua vinatembezwa na kigari maalum ndani ya treni, mtu yeyote akiwa
kwenye behewa lolote anaweza kutembea na kuingia kwenye behewa jingine,
vilevile kuna madaktari wameandaliwa kuhusika na huduma ya kwanza iwapo
itahitajika, pia pamoja na mambo mengine kuna behewa special ambalo
limetengwa kwa watu kupumzika.
No comments:
Post a Comment