Imefahamika kwamba rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela anaumwa maradhi ya mapafu lakini hali yake inaendelea vizuri.
Waziri wa ulinzi wa Afrika
kusini amesema hali ya mzee huyu wa miaka 94 ambae amelazwa kwenye
hospitali ya kijeshi Pretoria ni nzuri.
Amelazwa hospitali toka
jumamosi iliyopita kwa ajili ya vipimo ambavyo matokeo yake baadae
yalionyesha amepata maambukizi kwenye mapafu yake na sasa anatibiwa.
No comments:
Post a Comment