NSSF YADHAMINI TAMASHA LA 'TOTO PARTY' LITAKALOFANYIKA DESEMBA 25 NA 26 CINE CLUB, DAR
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamini tamasha la watoto
lijulikanalo kwa jina la 'Toto Party' linalotarajiwa kufanyika Desemba
25 na 26 mwaka huu katika ufukwe wa Cine Club jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited, ambao
ni waandaaji wa tamasha la TOTO PARTY, Bw. Dennis Ssebo alisema kuwa
anawashukuru NSSF kwa kuwaunga mkono na kuongeza udhamini wao kwa
tamasha hilo la Toto Party'
“Nawashukuru
sana Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuungana na sisi
katika kutoa burudani ambayo itawafikia watu wengi zaidi katika sherehe
za Noeli na Boxing Day”, Alisema Bw. Ssebo.
Katika
sherehe hizo mbili NSSF watatoa zawadi za vitabu pamoja na karamu kwa
kila mtoto atakayehudhuria vile vile watapata kucheza michezo mbalimbali
kama soka la ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na
kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Mbali
na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao
watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo
hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto
na wakubwa Sh 7,000.
Waratibu
wa sherehe pia wamebainisha kuwa mwakani mbali na Dar es Salaam,
sherehe hizo pia zitafanyika kwenye katika mikoa ya Arusha na Tanga.
No comments:
Post a Comment