Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.
Na Mwandishi Wetu
FAINALI za shindano la
kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ 2012, limemalizika
usiku wa kuamkia leo huku Catherine Masumbigana akishinda taji hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa
New Maisha Club, Oysterbay, jijini Dar
es Salaam.
Shindano hilo lililokuwa
likiwaniwa na warembo 12, ambao waliweza
kuonesha mavazi mbalimbali ikiwemo ya
ubunifu, usiku na mengineyo warembo hao
pia waliweza kukonga nyoyo kwa kuonesha uwezo wao wa kuimba na kucheza.
Majaji wa shindano hilo,
Gymkhana Hilal, Martin Kadinda na chifu jaji,
Asia Idarous walikuwa kwenye wakati mgumu kuchagua mshindi kutokana na
warembo wote kuwa na sifa za juu ambao baadaye walichuja na kubakisha watano kabla
ya kubaki watatu.
Chifu Jaji wa shindano hilo, Asia Idarous ndiye
alimtaja Catherine Masumbigana kuwa ndiye mshindi na kuufanya ukumbi kulipuka
kwa shangwe za wapenzi na mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini huku nafasi
ya pili ikienda kwa
Cesilia Michael na Amina
Ayubu akiwa wa tatu.
Mbali ya washindi hao, pia
taji la Unique Model Photogenic lilinyakuliwa na Elizabeth Pertty huku Unique Model Talent litwaliwa na Vestina
Charles.
Awali, akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza fainali hiyo, Mkurugenzi
wa Unique Entertainment inayoratibu shindano hilo,
Methuselah Magese aliwashukuru wadau mbalimbali
kwa kufanikisha shindano hilo
mpaka hapo lilipofikia.
“Nashukuru sana wadhamini wa shindano hili kwa kutuunga
mkono mara kwa mara, na tutaendelea kuleta mambo makubwa zaidi katika tasnia ya
mitindo na urembo nchini” alisema Magese.
Wahiriki walioshiriki
shindano hilo wengine ni Janecy Maluli, Judith Sangu, Darling Godfrey, Lulu
Mramba, Sadory Kendra, Elizabeth
Borniface na Zeenarth Habib ambao hawakufaniiwa kunyakua nafasi youyote.
Fainali hizo zilizodhaminiwa
na makampuni mbalimbali, zilisindikizwa na burudani kutoka kwa wanamuziki mahiri
waliokuwa kivutio kingine ukumbini hapo kwa kila mmoja.
Wadhamini wa fainali hiyo
walikuwa Free Media Ltd wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari,
Giraffe Ocean View, Kitwe General Traders, Sophanaa Investment, Dtv, Clouds Fm,
gazeti la Kiu, Mashujaa Investment Ltd, Blogu za Michuzi, Jiachie, Mtaa kwa
Mtaa, Unique Entertainment, Lamada Apartments & Hotel, Fabak Fashions,
Genesis Health Center na Yungdon Records, Paka Wear na Mtoko Design.
|
No comments:
Post a Comment