TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600 MWANZA
Mgeni rasmi
katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi,
akipanda mti wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji
hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni,
Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
Mgeni rasmi
katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi,
akipanda mti wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji
hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa
pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.
Mkurugenzi wa
Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo,
akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya
upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni
Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni
Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30
kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa
wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
Meneja wa TBL
Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa
upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni
hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta,
machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia
cha kampuni hiyo.
Diwani wa
Kata ya Mkuyuni, ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus
Mabula , Lugo Fasheni akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji
miti unaotekelezwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini
Mwanza.
Afisa Misitu
Jiji la Mwanza, Kaombe Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa
mgeni rasmi , Henry Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa
mradi wa upandaji miti jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL)
Mwanza, Raymond Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano
wa Jamii na Sheria TBL, Steven Kilindo.
Mmoja wa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini
Mwanza juzi. TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika
mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia
sh. mil. 10 kupanda miti 2600