MATUKIO KATIKA PICHA TASWA FC NA TASWA QUEENS ZILIVYO ICHAPA KILIFLORA YA ARUSHA
Pamoja
na Mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, jana na uwanja wa Netoboli
na wa Mpira wa miguu TCC kujaa maji lakini bado timu za TASWA FC na
Netiboli ya TASWA Queens, ziliibuka na ushindi mnono katika Bonanza la
Pasaka dhidi ya timu ya Kiliflora
ya Arusha. Hapa wachezaji na viongozi wa timu hizo wakijitahidi kuondoa
maji katika uwanja wa Netiboli kabla ya kuanza kwa mtanange huo, ambao
ulimalizika kwa TASWA Queens kuibuka na ushindi wa mabao 28 -8. Picha
zote na Nasma Mafoto
Majuto Omari wa Taswa Fc (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Kiliflora ya Arusha, ambapo hadi mwisho Taswa Fc Iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Iman wa Taswa Queens, akitupia moja kati ya magoli 28 waliyofunga.
Mtanange unaendelea.....
Beki wa TASWA Fc Muhidin Sufiani (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Kiliflora ya Arusha.
Mchezo ukiendelea japo uwanja ulikuwa ukisumbua kwa utelezi....
Mafoto, akiondosha hatari.....
Utelezi ukiwasumbua wachezaji wa Netiboli, hapa mmoja akienda chini
Salum Jaba wa Taswa, akiondosha hatari....
Mtanange ukiendelea.....
Wachezaji wa Taswa Queens, wakiwa katika picha ya pamoja.....
Shafii Dauda (kulia) akiwania mpira na wachezaji wa Kiliflora ya Arusha
Kiliflora ya Arusha.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akiwa katika picha ya pamoja na Taswa Queens.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akiwa katika picha ya pamoja na Kiliflora ya Arusha.
Kinadada wakiendelea kuchuana.
Kipute kikiendelea..
Wakiendelea kuchuana katika uwanja wa TCC Chang'ombe.
No comments:
Post a Comment