CHALZ BABA AJITOLEA KUWASAPOTI BURE WALEMAVU WA SURVIVAL SISTERS, TAYARI AMESHAREKODI NAO SONGI MOJA NA VIDEO
Wasanii
wa Kundi la Survival Sisters, wakiwa jukwaani na Chalz Baba, katika
moja ya shoo yan na Bendi ya Mashujaa Ijumaa iliyopita.
*************************************
MWIMBAJI
na kiongozi wa bendi ya Mashujaa ya jijini Dar es Salaam, amejitolea
kuwasaidia wasanii wa muziki wa dansi ambao ni walemavu wanaojulikana
kwa jina la Survival Sisters, linaloundwa na wanadada watatu, lenye
maskani yake Jijini Dar es Salaam.
Wasanii hao ni pamoja na Lucy Samson, Irene Mmbeka na Latifah Abdallah, ambao wote ni walemavu.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Chalz Baba, alisema kuwa
tayari mpaka sasa wamesharekodi wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la
Siambiwi
Sisikii,
uliorekodiwa katika Studio ya Metro, na video yake iliyokamilika tangu
mwaka jana mwishoni ikirekodiwa katika studi za Kiumbe Video.
Wimbo huo pamoja na video tayari wameshausambaza katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni na inaendelea kufanya vizuri
Aidha
wasanii hao kwa kushirikia na Chalz Baba, wapo mbioni kukamilisha albam
yao itakayokuwa na jumla ya nyimbo Nane, ambayo itapewa jina baada ya
kukamilika, huku ikitarajiwa kukamilika mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.
Chalz
Baba, alisema kuwa mbali na yeye pia yupo katika mazungumzo na baadhi
ya wasanii wengine, ili waweze pia kuwasaidia wasanii hao katika albam
yao hiyo, ili kuweza kupata radha tofauti na kuweza kuuza na baadaye
waweze kufikia malengo yao.
Katika
kutambua umuhimu na kutambua mchango wa wasanii hao kaatika sanaa
kutokana na akujituma kwao tofauti na walemavu wengine, Chalz Baba
ameanzisha utaratibu wa kuzunguka nao katika baadhi ya shoo za bendi
hiyo ya Mashujaa, ambapo kila siku ya Ijumaa na Jumapili kufaanya nao
shoo ya pamoja katika Ukumbi wa Green Acres ulipo Victoria, ili waweze
angalau kujipatia pesa kidogo za kujikimu.
Kutokana
na hali halisi ya wasanii hao kutokuwa na uwezo wa kuingia Studio na
kujilipia, wamekuwa wakidhaminiwa na baadhi ya studio kwa kupewa ofa ya
kurekodi nyimbo kulingana na makubaliano na mwenye studio, na ndivyo
hivyo wanavyotarajia kukamilisha albam yao hiyo kwa nia hiyo katika
Studio mbalimbali zitakazojitolewa kuwasaidia.
Kundi
hilo tayari lilifanikiwa kurekodi nyimbo tatu siku za nyuma na mbili
kati ya hizo walizisambaza kwenye Vituo vya redio, lakini kwa bahati
mbaya hazikuweza kufanya vizuri na kuwatambulisha kama walivyotarajia na
sasa wanaamini kumpata msamaalia mwema kama Chalz Baba, sasa wanaweza
kutambuka katika anga za muziki wa dansi kupitia jina lake, alisema
mmoja wa wasanii haoLucy Samson.
Chalz
Baba, aliwahasa wananii wengine wenye uwezo kujitokeza na kuwasaadia
wasanii hao ambao wanauwezo wa kuimba na kushambulia jukwaa, ili waweze
kutoka na kutambulika hata ikibidi Kitaifa na Kimataifa.
''Nawahaomba
wanamuziki wenzangu na hata wasanii wa muziki wa Bongo Flava, wenye
uwezo kujitokeza kuwasaidia wasanii hawa ili nao wajihisi ni miongoni
mwa wanamuziki kama tulivyo sisi na waweze kutambulika zaidi katika kazi
zao''. alisema Chalz Baba
No comments:
Post a Comment