Mgombea urais katika uchaguzi
mkuu ujao wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema mashtaka yanayomkabili ya
uhalifu dhidi ya binaadamu katika Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC
hayatomzuia kuiongoza nchini hiyo kama atachaguliwa kuwa rais.
Kenyatta ambae ni naibu Waziri
Mkuu ameyasema hayo kwenye mdahalo wa kihistoria na wa kwanza kufanyika
nchini Kenya kwa kuhusisha wagombea wote nane wanaoutaka urais.
Katika mdahalo huo ambao
ulirushwa live na TV mbalimbali za ndani na nje ya Kenya, Waziri mkuu
Raila Odinga anayepewa nafasi kubwa ya kushinda kwa mujibu ya kura ya
maoni, amesema Kenya haiwezi kuongozwa na mtu alie mbali na Kenya ambapo
wengi wanaamini hiko kilikua kijembe kwa Uhuru ambae anamashtaka The
Hague.
Odinga alisema hiyo ishu
itasababisha changamoto kubwa kwa serikali kuendeshwa kwa kutumia
mtandao wa kijamii wa Skype kutokea The Hague iwapo rais atakaechaguliwa
ni mwenye mashtaka The Hague.
Mdahalo mwingine kama huo utafanyika tarehe 25 february 2013 ikiwa ni wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu March 4 2013.