Wednesday, June 26, 2013

ANAYETUPAMBA BLOG YETU NI:

 

Jina: Sarah Mlaye.

Elimu: Mwanafunzi wa Chuo, Saint Augustine University.

Hobby: Modelling.

Malengo: Kuwa Mtangazaji wa Kimataifa.

MBUNGE WA CHADEMA SUGU AKANA KUMUOMBA RADHI WAZIRI MKUU KWA KUMUITA "MPUMBAVU"



Juzi, mbunge wa mbeya mjini alitoa tusi zito kwa waziri mkuu wa Tanzania na kudai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbuvu kama yeye...

Kupitia account yake ya facebook, Sugu, ambaye ni mbunge wa mbeya amezidi kusisitiza kuwa hawezi kuomba msamaha wala kuifuta kauli yake....

Hii ni post yake facebook:

"...naskia kuwa watu wanasema kwamba eti nimefuta kauli yangu kuhusu waziri mkuu na amri yake kwa polisi kupiga wananchi?!...

Sina sababu ya kufuta wala kuomba radhi, na nasimamia kauli yangu to the end...kwanza 'upumbavu' sio tusi,upumbavu kwa kiingereza ni stupidity-which is lack of knowledge and understanding...

So hata uwe na cheo gani kama ukishindwa kuwa na 'understanding' juu ya madhara ya kauli zako kwa taifa then u r 'stupid'...ambapo kwa kiswahili ndio 'mpumbavu'..."

Ulinzi wa Obama haujawahi kutokea Afrika



Tayari baadhi ya wanajeshi wa Marekani wamewasili Dar es Salaam na kuweka mitambo ya mawasiliano maeneo yote ambayo atapita au kukagua.

Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.

Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.

Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.

Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.

Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.

Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.

Sala zetu kwa Mzee Madiba




Pamoja na mkutano huo, wanafamilia hao walifanya mazungumzo na machifu wa eneo hilo, wakiongozwa na Chifu Bhovulengwe wa Baraza la Kifalme la Abathembu.

Johannesburg. Familia ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela imesema haitaruhusu kusitishwa kwa matibabu anayoendelea kuyapata na kwamba itaendelea kufanya juhudi za kurefusha uhai wake hadi Mungu atakapoamua kumchukua.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mwanawe mkubwa, Makaziwe Mandela huku kukiwa na taarifa kwamba kiongozi huyo hajitambui na anasaidiwa kuendelea kuishi kwa mashine tangu alipofikishwa hospitalini huko Pretoria wiki mbili zilizopita.

Alisema kwamba familia haiwezi kuacha kumhudumia kwa shinikizo la watu wa pembeni wanaodai kwamba inatakiwa imruhusu akapumzike kwa amani na kwamba kwa mujibu wa mila za Wathembu, watafanya hivyo endapo tu mhusika mwenyewe (Madiba), atakapotamka.

Juzi, kwa mara ya kwanza, Rais Jacob Zuma alikiri hadharani kwamba hali ya shujaa huyo wa Afrika Kusini ni mbaya na anahitaji maombezi. Alisema hayo baada ya kumtembelea na kuzungumza na mkewe, Graca Machel-Mandela.

Hata hivyo, taarifa zilieleza kwamba hajaweza kuzungumza tangu alipofikishwa hospitali, bali alifungua macho kwa shida mara kadhaa.

Mandela anayesumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu alifikishwa katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo ya Medi-Clinic, Pretoria Juni 8 na tangu wakati huo, taarifa zimeeleza kwamba hajaweza kuzungumza lolote.

Taarifa zikieleza kwamba hali yake ilizidi kuwa mbaya Jumapili iliyopita na baadhi ya wanafamilia tayari wameshatangulia kijijini kwake, Qunu.

Gazeti la Mail&Guardian la Afrika Kusini lilieleza jana kwamba wanafamilia hao walifanya kikao maalumu nyumbani kwa Mandela, kisha kutembelea na kufanya ukaguzi katika eneo la makaburi ya familia, sehemu ambayo kiongozi huyo pia anaweza kuzikwa.

Makaburi hayo yako jirani na nyumba ya mdogo wake, Morris na haikuwekwa wazi kuhusu uamuzi wa wanafamilia hao kufika eneo hilo la makaburi, lakini kwa mujibu wa mila na desturi za watu wa Kabila la Xosa, familia hutembelea eneo hilo wanapobaini kwamba mmoja wa wanafamilia yuko mbioni kuungana na waliotangulia mbele za haki, au kuomba sala maalumu kwa ajili ya kupata ridhaa ya kurefusha maisha ya mhusika.

Pamoja na mkutano huo, wanafamilia hao walifanya mazungumzo na machifu wa eneo hilo, wakiongozwa na Chifu Bhovulengwe wa Baraza la Kifalme la Abathembu.

Wanafamilia waliofika na kuhudhuria kikao hicho cha jana ni pamoja na mkewe wa zamani, Winnie Madikizela-Mandela na Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala, Lindiwe Sisulu pamoja na Kiongozi wa Chama cha United Democratic Movement, Bantu Holomisa.

Iliarifiwa kwamba kikao hicho kilifanyika kutokana na simu ya dharura iliyopigwa kwa wanandugu na wanawe, Mandla, Thanduxolo, Ndaba na Ndileka Mandela ambao tayari walishawasili kijijini hapo tangu Jumapili na kujumuika na wanafamilia wengine.

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERIA



Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.

Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.

Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.

Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.

Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria.

Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.

Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.

Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”

Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.

“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.

“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).

Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.

Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.
“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.

Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.

MAAJABU YA DUNIA HAYA JAMANI: MTOTO MMOJA MCHAWI KUTOKA SHIRIKA MOJA LA KIDINI KULEA WATOTO MKOANI IRINGA AKAMATWA NA KUCHOMEWA VITU VYAKE VYA UCHAWI!!!



Hapa mtoto Naomi akitoa vifaa vyake vya Uchawi

Ni jambo la kusikitisha na la kweli lililotokea katika kata ya Kihesa Mkoani Iringa, Mtoto mmoja kwa jina la Naomi ambaye analelewa na shirika lisilo la kiserikali la Compassion,Kituo cha Kihesa amestaajabisha jamii kwa kukutwa na vitu vya Kichawi nyumbani kwao pasipo mama yake kufahamu chochote.

Chanzo chetu cha habari kimetutonya kuwa mtoto huyo alikuwa na mambo yasiyo ya kawaida tangu muda mrefu sana,Kwanza maendeleo yake shuleni ni hafifu pia ana tabia ya kutoloka nyumbani au shuleni na kuelekea pahali asipopajua.

Wakati mwingine huwa anakutwa umbali mrefu sana akiwa amezubaa tu njiani hana uelekeo, Chanzo kinasema kuwa wakati wa maombi mototo huyo huwa kama ni mtu aliyezama sana kwenye maombi na hupenda sana kuimbisha nyimbo za kumsifu Mungu.

Chanzo chetu kinaendelea kusema kuwa mtoto huyu amekuwa ni kero kwa mama yake kwa tabia yake ya kutorokatoroka nyumbani na shuleni.

Chanzo kinasema kuwa ilikuwa ni siku ya jumamosi ambapo watoto wote wanaonufaika na huduma hiyo hukutanika kwa ajili ya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kiroho, Siku hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya maombi ya pamoja na vituo vingine yaliyofanyika katika kanisa la kristo mfalme Mjini Iringa mtoto huyo hakuwepo katika orodha ya kati ya watoto waliochaguliwa katika msafara huo na mara nyingi katika matukio kama hayo ya kutoka nje ya kituo huwa ni king’ang’anizi sana hata akiachwa hukutwa katika eneo la tukio nailikua ikizaniwa ametembea kwa mguu kufika hapo.

Siku hiyo ilikua ya kushangaza kidogo kwani walihakikisha amezuiwa na kuachwa kituoni lakini walipofika tu getini kristo mfalme umbali wa kilomita 7 walimkuta mtoto huyo ameshafika na ilipopigwa simu kituoni kuuliza kama yupo wakasema sio mda mchache ameonekana kule alipoulizwa amefikaje akasema amefika kwa mbinu zake ndipo jopo la wanamaombi likakusanyika na kumfanyia maombi.

Baada ya hapo wanamaombi wakaelekea nyumbani kwa mtoto na kutoa vitu mbali mbali vya kishirikina kama kisu,wembe,msumali, sindano ,sahani na vinginevyo alivyokua akitumia kuulia watu na kuwawangia watoto wenzake kituoni hapo na alifanikiwa kuwapata watoto wanne ambao alikua anafanyanao mambo ya kichawi.Hata hivyo kila siku ikifika mida ya saa tisa mchana amekua akila nyama za watu na kula damu za watu. Pia amekua akifanya mapenzi na majini kumi na mbili kwa siku.

Baada ya hapo likafuatia tukio la kuchoma moto vitu vyake katika ile sehemu yake ya kuondokea kwenda kufanya shughuli zake za kichawi.



Hapa ni sehemu yake ya kuondokea kwenda kufanya uchawi vitu vyake vikiwa vinaungua baada ya kuchomwa moto

Hapa wanamaombi wakivichoma moto vitu vya Kichawi vya Naomi

FAMILIA YA MATUMLA YALALAMIKIA UMASKINI


Bondia Rashid Matumla alipotwaa ubingwa wa dunia wa WBU
Bondia Mbwana Matumla enzi zake alipokuwa akitamba katika ndondi za kulipwa na Bondia Hassan Matumla  alipokuwa akipigana masumbwi ya kulipwa

UNAPOZUNGUMZIA ngumi za kulipwa ama za ridhaa hapa nchini, si rahisi kuacha kulitaja jina ama ukoo wa Matumla. Ni familia ya mabondia walioweza kulitangaza vyema jina la Tanzania kimataifa tangu walipokuwa wakipigana ndondi za ridhaa hadi walipohamia kwenye ndondi za kulipwa.

 
Ni familia ya mzee Ally Matumla, inayoundwa na watoto zaidi ya 10, wakiwemo wawili wa kike, lakini ni wachache walioweza kuchomoza vyema katika mchezo huo, wakifuata nyayo za kaka yao, Rashid Matumla na Ally Matumla, ambaye kwa sasa ni marehemu.

 
Watoto wengine wa mzee Matumla walioweza kulitangaza vyema jina la Tanzania kimataifa kupitia ndondi za ridhaa za kulipwa ni Mbwana, Haji, Karim, Hassan, Mkwanda.

 
Hata hivyo, mtoto pekee aliyeweza kulitangaza vyema jina la familia hiyo ni Rashid, ambaye baada ya kung'ara kwenye ndondi za ridhaa miaka ya 1980, ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na kushiriki Michezo ya Jumuia ya Madola na Michezo ya Olimpiki, aliamua kuhamia kwenye masumbwi ya kulipwa.

 
Ni katika ngumi hizo, ndipo Rashid alipoweza kuonyesha umahiri wake kwa kutwaa ubingwa wa Afrika, mabara, mkanda wa kimataifa na wa dunia, yote yakiwa chini ya WBU. Katika kipindi chote hicho, Rashid alikuwa akipigana chini ya udhamini wa Kampuni ya DJB Promotions, inayomilikiwa na Jamal Malinzi.

 
Licha ya kutangaza mara kwa mara kwamba atastaafu mchezo huo, Rashid bado anaendelea kuzipiga katika mapambano ya kulipwa na mara ya mwisho alidundwa kwa pointi na mpinzani wake wa jadi, Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo'.

 
Kinachomfanya Rashid ashindwe kustaafu mchezo huo ni kuwepo kwenye damu yake. Anasema kila mara anajisikia hamu ya kupigana, si tu kutokana na mapenzi yake kwa mchezo huo, bali pia kujipatia riziki ya kuendesha maisha yake ya kila siku.

 
Kwa upande wake, Hassan ameshastaafu mchezo huo baada ya kuvunjika kidole cha mkono wake wa kushoto. Mbwana bado anaendelea kupigana, lakini si kwa kiwango alichokuwa nacho zamani, ambacho kilimvutia kocha Nolman Hlabane wa Afrika Kusini, aliyeamua kumchukua na kumtafutia promota nchini humo.

 
Mkwanda kwa sasa anaishi Sweden, ambako bado anaendelea kucheza ngumi za kulipwa wakati Karim aliamua kuzamia nchini Australia miaka kadhaa iliyopita alipokwenda huko kushiriki Michezo ya Jumuia ya Madola. Tayari Karim ameshacheza mapambano matatu ya kulipwa na kushinda yote.

 
Licha ya kushiriki katika ndondi hizo kwa miaka mingi, Rashid, Hassan na Mbwana wamekiri kuwa, hawana lolote la maana la kujivunia katika maisha yao zaidi ya kuambulia sifa kutokana na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

 
Wanafamilia hao watatu wa ukoo wa Matumla, walisema hayo wiki iliyopita walipokuwa wakihojiwa katika kipindi cha Mkasi kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Channel Five.

 
"Kama familia yetu ingekuwa inaishi Marekani, nadhani tungekuwa matajiri sana,"alisema Rashid wakati wa mahojiano hayo.

 
"Familia yetu ni maarufu kwa mchezo wa ngumi, lakini ni maskini. Maisha tunayoishi, siyo yale tuliyopaswa kuishi," aliongeza bondia huyo, ambaye aliwahi kupigana nchini Hungary na Italia na kuwadunda mabondia kadhaa wa nchi hizo katika mapambano ya uzani wa middle.

 
Pamoja na kutopata mafanikio makubwa kimaisha kutokana na mchezo wa ndondi, Hassan alisema lengo lao kubwa ni kuupromoti mchezo huo kwa lengo la kuibua vipaji vya mabondia chipukizi na kuwaendeleza.

 
Kwa mujibu wa Hassan, tayari wameshaanza kusaka ufadhili kwa ajili ya kutimiza lengo lao hilo na kuongeza kuwa, wanatarajia kuianza kazi hiyo hivi karibuni.

 
Hassan alisema kukosekana kwa ufadhili ndiko kunakosababisha bondia kama vile Francis Cheka, ambaye amekuwa akifanya vizuri hapa nchini, kushindwa kwenda nje kuwania mikanda ya kimataifa, kama ilivyokuwa kwa Rashid, alipokuwa chini ya DJB Promotions.

 
Alisema Cheka ni bondia mzuri, lakini uzuri wake umekuwa ukiishia ndani ya mipaka ya Tanzania bila ya kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake kimataifa. Alisema ana hakika iwapo Cheka angepata udhamini wa uhakika, angeweza kutwaa ubingwa wa dunia.

 
Cheka ndiye bondia pekee nchini aliyewahi kuwadunda mabondia kutoka familia ya Matumla. Alianza kuonyesha umwamba wake kwa Rashid kabla ya kumdunda Hassan. Hakuna bondia wa familia hiyo aliyeweza kumdunda Cheka.

 
Kwa upande wake, Mbwana aliitaja faida pekee, ambayo familia yao wameweza kuipata kuwa ni kuajiriwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kupitia mchezo wa ndondi. Wapo walioajiriwa katika Jeshi la Polisi na wengine Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 
"Tuliweza kupata ajira kirahisi kwenye vyombo vya usalama kwa sababu ndiko kulikokuwa rahisi kuajiriwa kupitia michezo. Karibu sisi sote tulikuwa askari,"alisema Mbwana.

 
Akizungumzia udhamini wa ndondi za kulipwa ulivyokuwa enzi zake, Rashid alisema ulikuwa mzuri na wa uhakika na kuongeza kuwa, hakuwahi kusumbuliwa ama kudhulumiwa haki zake na mapromota.

 
Alimtaja promota Phillemon Kyando 'Don King' kuwa ndiye aliyemwingiza kwenye ndondi za kulipwa na kumsaidia mambo mengi kabla ya kuchukuliwa na Malinzi, ambaye alimwendeleza zaidi kwa kumwandalia mapambano ya kimataifa.

 
"Kusema ule ukweli, tangu nilipoanza kupigana ndondi za kulipwa, sijawahi kugombana na promota yeyote. Walikuwa wakinitimizia na kunipatia kila nilichokuwa nikikihitaji,"alisema Rashid.

 
Alipoulizwa sababu ya Tanzania kufanya vibaya katika mashindano ya kimataifa ya ndondi za ridhaa, Rashid alisema ni kutokana na maandalizi duni na ya zimamoto. 

 
Rashid alisema mara nyingi mabondia wa Tanzania wanaoshiriki kwenye mashindano ya kimataifa wamekuwa wakipelekwa kambini miezi michache kabla ya kwenda kushindana na hivyo kukosa uzoefu wa kutosha.

 
Alisema ni vigumu kwa bondia anayekwenda kushindana katika Michezo ya Olimpiki na Jumuia ya Madola kuweza kufanya vizuri iwapo hatapata maandalizi ya kutosha na ya muda mrefu.

 
Rashid kwa sasa anao watoto wanne, mmoja akiwa amerithi kipaji chake. Mtoto wake huyo wa kwanza anajulikana kwa jina la Mohamed na hivi karibuni alimdunda mtoto wa Cheka, Cosmas Cheka kwa pointi walipozipiga mjini Morogoro, ikiwa ni kulipiza kisasi cha vipigo walivyopata baba zake, Rashid na Hassan.

Hawa ndiyo visura wa Redd's Miss Temeke 2013

 Mrembo Jamila Ramadhan, akiwa katika pozi.
 Mrembo Hyness Oscar, akiwa katika pozi.
 Mrembo Margreth Olotu, akiwa katika pozi.
 Mrembo Latifa Mohamed, akiwa katika pozi.
 Mrembo Mutesi George, akiwa katika pozi.
 Mrembo Mey Karume, akiwa katika pozi.
 Mrembo Stella Mgazija, akiwa katika pozi.
 Mrembo Margreth Gerrad, akiwa katika pozi.
 Mrembo Axsaritha Vedastus, akiwa katika pozi.
 Mrembo Naima Ramadhan, akiwa katika pozi.
 Mrembo Irine Rajab, akiwa katika pozi.
 Mrembo Eastear Msulwa, akiwa katika pozi.
 Mrembo Svtlona Nyameyo, akiwa katika pozi.
 Mrembo Darlin Mmari, akiwa katika pozi.

Mrembo Narietha Boniface, akiwa katika pozi.


Baadhi ya washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao juzi.
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao. Kutoka kushoto, waliosimama ni Magreth OlotuNarieth Boniface, Latifa Mohamed, Mutesi George, Naima Ramadhan, Axarith Vedastus, Mey Karume, Easter Msulwa, Margreth Gerrad, Svtlon Nyameyo na walikaa chini ni Hyness Oscar, Jamila Ramadhan, Irine Rajab, Stella Mgazija na Darlin Mmari.
Baadhi ya warembo hao, wakipozi kwa picha kwenye mazoezi yao
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao. Kutoka kushoto, waliosimama ni Magreth Olotu, Narieth Boniface, Latifa Mohamed, Mutesi George, Naima Ramadhan, Axarith Vedastus, Mey Karume, Easter Msulwa, Margreth Gerrad, Svtlon Nyameyo na walikaa chini ni Hyness Oscar, Jamila Ramadhan, Irine Rajab, Stella Mgazija na Darlin Mmari .

Joh Makini kukumbatia Ambassadors Lounge Ijumaa hii

Yusuph Mlela aibukia kwa Miss Serena

Yusuph Mlela katika pozi
 MSANII mahiri wa filamu nchini, Yusuph Mlela 'Angelo' anajiandaa kuingiza sokoni filamu yake mpya iitwayo 'Miss Serena' ambayo ameifyatua chini ya kampuni yake binafsi iitwayo 'Mlela Films Production'.

Akizungumza na MICHARAZO, Mlela alisema filamu hiyoi aliyoigiza na wakali wenzake kama Salma Jabu 'Nisha' , Sabrina Rupia 'Cathy' na Seleman Abdallah 'Barafu' ipo katika maandalizi ya kuwachiwa wakati wowote kuanzia sasa.


Mlela alisema filamu hiyo ya kimapenzi na yenye mafunzo kwa jamii ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yake tangu alipoianzisha hivi karibu kama njia ya kujikomboa.


"Kaka nimekamilisha filamu yangu mpya ambayo ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yangu na itafahamika kwa jina la 'Miss Serena' ambapo imewashirikisha wakali kadhaa nikiwemo mimi mwenyewe, Nisha, Barafu na Cathy wa Kaole," alisema Mlela.


Mlela aliyetambulishwa kwenye ulimwengu wa filamu mwaka 2006 kupitia filamu ya 'Diversion of Love' kabla ya kujipatia umaarufu katika filamu zaidi ya 30 alizocheza mpaka sasa alisema kazi hiyo mpya ni moja ya kazi nzuri alizozalisha baada ya kutoa Angel na Poor Minds.


Mkali huyo ambaye pia ni mwanamitindo alisema mashabiki wake wakae mkao wa kula kupata burudani kabambe wakati akiwa 'location' kwa sasa akishirikishwa kwenye kazi mpya ya Wastara Juma 'Stara'.

TEVEZ APATA MAPOKEZI MAKUBWA ITALIA TAZAMA PICHA

tevez2 403cfCarlos Tevez kushoto akiwasili jijini Turitevez4 7dfa1
tevez 2fa1b
tevvez3 90137
MSHAMBULIAJI Carlos Tevez amewasili Italia na kupata mapokezi makubwa kuelekea uhamisho wake wa Pauni Milioni 10 Juventus kutoka Manchester City.
Mpachika mabao huyo wa Kiargentina alitua katika Uwanja wa Ndege wa Malpensa mjini Milan na kupokewa na umati wa mashabiki ambao mara zote hupenda kuwalaki nyota wao wapya.
Tevez, mwenye umri wa miaka 29, anataraji kusaini mkataba wa miaka mitatu jijini Turin baada ya vipimo vya leo huku makubaliano yakiwa yamefikiwa. Chanzo: Sportmail

HALI YAZIDI KUWA TETE KATIKA CHUO KIKUU CHA TEOFELO KISANJI, UONGOZI WA CHUO NAO WATOA TAMKO .

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari.

 Waandishi wa Habari wakiwa nje ya ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo kwa zaidi ya Masaa Matatu
 Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari
 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofelo kisanji wakingoja kusikia Hatima yao


Hali bado ni tete katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha Mgomo huo.
 
Akisoma Tamko la kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
 
Hata hivyo Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.

Ameongeza kuwa kama  kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya kubatilisha.

JESHI LA POLISI LATOA ONYO LA KUTOFANYIKA KWA MAANDAMANO YA CUF KWENDA IKULU DAR ES SALAAM


Jeshi la polisi limetoa onyo la kutofanyika maandamano ya CUF kwenda Ikulu na endapo watalazimisha kuandamana hatua za kisheria zitachukuliwa. Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam CP Suleiman Kova amesema Tanzania itakua mwenyeji wa ugeni mkubwa wa kimataifa ukiwemo wa ushirikiano kwa manufaa ya wote ambao utahusisha maraisi 14.

TIGO KUFANYA TAMASHA KUBWA LA KABANG JUMAPILI HII NDANI YA CCM KIRUMBA MWANZA

 Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa katika viwanja vya  CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond Platnumz na kulia msanii Madee ambao watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine.
 Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga.
 Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz .
  Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz.
Wasanii Diamond Platinumz, Madee wa Tip Top na Richie Mavoko katika picha ya pamoja na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga. Wasanii wengine watakaokuwepo ni Fid Q,  Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Recho na Kazi Kwanza.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
        
Tamasha la Tigo Mini Kabaang kufanyika jijini Mwanza
Dar es Salaam, Juni 26, 2013 – Msanii Bora wa mwaka Diamond Platnumz, Fid Q na wasanii wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na wateja wao kwa  kutumia sanaa ya muziki kama njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja wengi zaidi.

“Tunaamini kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na wateja wetu kuelewana zaidi.  Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema Mpinga.

Mini Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku. 

Mkutano huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumamosi katika viwanja vya CCM Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

“Mimi pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu tamasha hilo.

“Binafsi nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha  mapenzi ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,” aliongeza super staa huyo. 

“Tamasha hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.

“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika 20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.

Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.

KUHUSU TIGO:

Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania bara na visiwani.

Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.

Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani
Afrika na Amerika ya Kusini.

"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Amani Nkurlu – Meneja Mahusiano

+255 658 870 107 au +255 712 223 839